Monday 27 May 2013

HICHI NDICHO WALICHO SEMA WAHIRIKI WA BBA KUTOKA TZ

Mrembo Feza na mtanashati Nando Ndani ya jumba la Big Brother Africa
Haya, Big Brother Africa the Chase ndio hiyo tena kwenye runinga zetu, washiriki 28 kutoka nchi 14 tayari wameshaingia kuziwakilisha nchi zao. Kutoka Tanzania yupo mrembo Feza na mtanashati Nando..
Wakifunguka kwa Biggie, hivi ndivyo Feza na Nando walivyojielezea:

Feza
Feza (25) ni msanii lakini pia ana cheti cha IT. Anapendelea kiepe (chips), ugali na maziwa. Feza amejiunga na BBA kwa sababu anaamini ni muhimu kwa kazi yake kwani wengi wanaoshiriki BBA, kwa mtazamo wake, wanafanikiwa baadaye. Mrembo huyo anasema akishinda pesa hiyo atawekeza kiasi, atampeleka mwanae Disneyland na pengine kujinunulia nyumba.
Feza hapendi watu waongo. Anajielezea kama mcheshi, mkarimu na mpambanaji… amewaahidi watazamaji kucheza muziki, kupiga kelele na kucheka kwa sana tu.
Mrembo huyu anamtaja mama yake kama Role Model wake.

Nando
Nando (22) ni mwanafunzi. Mtanashati huyu anaelezea kwamba hajawahi kuangalia BBA kabla bali alishawishiwa na marafiki zake na anasikia poa tu kwamba bara zima litakua likimtizama masaa 24.
Nando anajielezea kama ‘kijana mwenye malengo, mcheshi na mkarimu, na anapendelea watu wenye roho safi na wasikivu. Kwa Tanzania, Nando anataja kuupenda zaidi mji wa Arusha na ulimwenguni anakupenda Brazil. Nando akishinda kitita hicho anasema atajenga ‘empire’.
Kuhusu chakula, Nando anapenda misosi aina zote, anapenda muziki na show ya TV anayopendelea ni ‘1000 ways to die’. Mwakilishi huyu wa Tanzania anapenda pia mpira wa miguu.
Tanzania, the chase for $300,000 is on.. Kura kura kura ni muhimu sana kuendelea kuwaweka watanzania hawa kwenye ma-rubies na ma-diamonds.

No comments: