Friday 10 May 2013

YANGA KUKABIDHIWA KOMBE KATIKA MECHI DHIDI YA SIMBA


 
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) litakabidhi kombe kwa mabingwa wapya wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Yanga katika mechi yao ya mwisho ya ligi hiyo dhidi ya mahasimu wao wa jadi, Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Mei 18.

Akizungumza na NIPASHE jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi ya TFF, Wallace Karia alisema kuwa wataikabidhi Yanga kombe hilo baada ya kumalizika kwa mechi hiyo ya kufunga msimu wa 2012/13 wa ligi

No comments: