Wednesday 29 May 2013

NANDO MSHIRIKI WA TZ BBA AOMBA WANAWAKE WAZURI WAONGEZWE BBA

Nando aomba warembo zaidi

Akiongea na baba mwenye nyumba kupitia Diary Session, mtanzania Nando alitoa ombi ambalo halikutarajiwa, kimsingi aliomba wanawake waongezwe akipendekeza watoke Ruby house.

Big brother alipomuuliza kuhusu kuwepo kwa wasichana Diamond house wa kutosha, Nando alijibu, ‘Nawapenda wasichana walioko Diamond house lakini ningependa kuzungukwa na warembo zaidi hasa wale walioko Ruby house”

Nando ni kijana mtanashati kutoka Tanzania na inaonekana dhahiri anafurahia uwepo na wasichana wengi tofauti tofauti ili aweze kufanya chaguzi yakinifu. Hasemi moja kwa moja lakini kwa mtazamo, pengine mbinu yake ya kuicheza game ikategemea kwa kiwango kikubwa uwepo wa wasichana wengi mbalimbali.

Katika hatua nyingine Big brother ametikisa upepo, harufu nzuri ya mapendo inanukia mjengoni. Baada ya kuwaacha washiriki wafahamiane kwa siku chache, wiki hii baba mwenye nyumba huyo amewataka watengeneze zawadi ya malavi davi ambayo kila mmoja atamkabidhi ampendaye kwa siri (secret crush) mjengoni humo siku ya Alhamis usiku.

Itakuwa burudani sana kuona nani atampa nani zawadi na wengine watajisikiaje. Bila shaka, mawivu na maumbea yatahusika kwa asilimia kubwa. 

Big brother ndo hivyo tena ameshatikisa kiberiti.. Endelea kufuatilia kufahamu nini kitatokea...

** Jumba la Big Brother Africa kwa msimu huu limegawanywa kuwa nyumba mbili ambazo ni Ruby House na Diamond House. Kila nyumba ina washiriki 14. **Nando aomba warembo zaidi
Akiongea na baba mwenye nyumba kupitia Diary Session, mtanzania Nando alitoa ombi ambalo halikutarajiwa, kimsingi aliomba wanawake waongezwe akipendekeza watoke Ruby house.
Big brother alipomuuliza kuhusu kuwepo kwa wasichana Diamond house wa kutosha, Nando alijibu, ‘Nawapenda wasichana walioko Diamond house lakini ningependa kuzungukwa na warembo zaidi hasa wale walioko Ruby house”
Nando ni kijana mtanashati kutoka Tanzania na inaonekana dhahiri anafurahia uwepo na wasichana wengi tofauti tofauti ili aweze kufanya chaguzi yakinifu. Hasemi moja kwa moja lakini kwa mtazamo, pengine mbinu yake ya kuicheza game ikategemea kwa kiwango kikubwa uwepo wa wasichana wengi mbalimbali.
Katika hatua nyingine Big brother ametikisa upepo, harufu nzuri ya mapendo inanukia mjengoni. Baada ya kuwaacha washiriki wafahamiane kwa siku chache, wiki hii baba mwenye nyumba huyo amewataka watengeneze zawadi ya malavi davi ambayo kila mmoja atamkabidhi ampendaye kwa siri (secret crush) mjengoni humo siku ya Alhamis usiku.
Itakuwa burudani sana kuona nani atampa nani zawadi na wengine watajisikiaje. Bila shaka, mawivu na maumbea yatahusika kwa asilimia kubwa.
Big brother ndo hivyo tena ameshatikisa kiberiti.. Endelea kufuatilia kufahamu nini kitatokea...
** Jumba la Big Brother Africa kwa msimu huu limegawanywa kuwa nyumba mbili ambazo ni Ruby House na Diamond House. Kila nyumba ina washiriki 14. **

No comments: