Monday 20 May 2013

Kabula adaiwa kumpa penzi Tegete wa Yanga

Staa wa sanaa za maigizo Bongo, Miriam Jolwa ‘Jini Kabula’, amedaiwa kutoka kimapenzi na straika wa Yanga, Jerry Tegete.

Sababu ya kuibuka kwa madai hayo ni Kabula mwenyewe, pale alipoitundika picha ya Tegete kwenye akaunti yake ya mtandao wa watumia Blackberry (BBM).





Baada ya Kabula kuiweka picha hiyo, watu mbalimbali wenye uwezo wa kuifikia akaunti yake, walimpongeza kwa kujiweka kwa janki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kuzitikisa nyavu.
Huku wengine wakimpongeza, baadhi walimhoji kama ameachana na mwanamuziki nguli wa Bongo Fleva, Ruta Maximilian Bushoke.
Hata hivyo, baada ya kuona anapokea ujumbe kutoka kwa watu wengi ambao moja kwa moja walihitimisha kwamba anatoka kimapenzi na Tegete, Kabula aliamua kuwaka.
Kabula, alisambaza ujumbe kwa watu wote wanaoweza kuifikia akaunti yake na kufafanua kuwa hana uhusiano na Tegete ila anamkubali ndiyo maana ya kuweka picha hiyo kwenye ukurasa wake.
“Jamani hivi siwezi kuweka picha ya mwanaume kwenye DP yangu mpaka awe mwanaume wangu. Nimeweka picha ya picha ya Tegete kwa sababu namkubali, siyo mpenzi wangu,” alisema Kabula.

No comments: