Monday 20 May 2013

kikombe cha mpa babu zaidi ya blioni mbili nyumba nzuri na gari la kifahari


 

 



 
Na Mwandishi Wetu
MAMBO yamemnyookea Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Masapile ‘Babu Ambi’ (pichani) na tayari ameanza kuonesha jeuri ya fedha nyumbani kwake Samunge, Loliondo.

Nyumba ya kifahari yenye thamani ya shilingi milioni 100 inajengwa na ndiyo itakuwa makazi mapya ya Babu Ambi.

Kwa mujibu wa ramani ya nyumba hiyo, mbali na makazi ya Babu Ambi, pia kutakuwa na maeneo yaliyojengwa kisasa kwa ajili ya kutolea huduma ya kikombe na kupumzika wagonjwa.

Askofu Mkuu wa KKT, Dayosisi ya Kaskazini, Thomas Laizer aliliambia Uwazi wiki iliyopita kuwa maandalizi ya ujenzi yameshaanza. 

Laizer alisema, ujenzi huo ukikamilika, utamaliza adha ya Babu Ambi kuishi kwenye nyumba chakavu ambayo anaishi hivi sasa.

“Ujenzi wa nyumba hiyo unasimamiwa na KKKT,” alisema Laizer na kuongeza: “Ramani ya jengo  hilo  ni nzuri na ni la kisasa.”

Aliendelea kusema: “Nyumba itajengwa kulingana na ramani iliyopo hata kama hivi sasa wagonjwa wamepungua.”

Aliongeza kuwa nyumba hiyo itakuwa na huduma zote muhimu, ikiwemo umeme na maji hivyo kuking’arisha Kijiji cha Samunge.

HUENDA NYUMBA IKAPUNGUZWA
Askofu Laizer alisema, ramani ya nyumba hiyo ni kubwa na inaendana na mahitaji ya mwanzoni, wakati huo Babu Ambi alikuwa na uwezo wa kuhudumia wagonjwa 24,000 kwa siku.

“Hapa katikati  idadi ilipungua ikawa wanaofika Samunge ni kati ya watu 8,000 hadi 9,000. Hivi sasa idadi imeshuka tena, kwa siku wanaofika Samunge ni 2,500,” alisema Laizer na kuongeza:

“Ikiwa watu watapungua zaidi na kufikia kati ya 1,000 na 500, itabidi tupunguze ukubwa wa jengo. Haitakuwa sawa kujenga nyumba kubwa kuliko mahitaji.”

AENDELEA KUKIFAGILIA KIKOMBE
Laizer alisema, kikombe cha Babu kinatibu, tatizo kuna watu wachache wanaomponda ambao wanaamini amewaingilia kwenye biashara zao.

“Wengine ni wivu tu wa kibinadamu kwa kuona kuwa wateja wao wanakwenda kwa Babu. Huduma anayoitoa Masapile ni ya maombi na imani, wengi wameshuhudia kupona baada ya kunywa dawa ya Babu,” alisema.

ASHAURI WATU WASIACHE DAWA ZA HOSPITALI
Askofu Laizer alisema: “Hii huduma haizuii watu wasife mbona hata hospitalini wagonjwa wanakufa?  Wale waliokufa wengi waliacha kutumia dawa za kurefusha maisha, ARV.

“Sisi hatukuwaambia wasiendelee kutumia dawa za hospitali, isipokuwa wao wenyewe waliamua kuacha. Na madaktari ambao wanasema dawa ya Babu imeua watu wengi, inabidi wafanye kwanza uchunguzi. Kuna dawa nyingi zinatibu na hazipitii hospitali.

“Mimi niipongeze serikali yetu, kwa kweli imefanya kazi kubwa ikiwemo kuratibu watu na kuwapanga, kuhakikisha hawachukui muda mrefu.”

KIKOMBE CHAINGIZA SHILINGI BILIONI MBILI
Kwa mujibu wa Askofu Laizer, mpaka sasa watu waliokwenda Samunge na kuhudumiwa kikombe wamefikia zaidi ya milioni nne.

Kwa hesabu hiyo, watu milioni nne kwa shilingi 500 kwa kichwa, inamaana kuwa kikombe cha Babu kimeshaingiza zaidi ya shilingi bilioni mbili.

GARI LA KIFAHARI HILO
Pamoja na Askofu Laizer kushindwa kulifafanua hilo, habari zinasema kuwa gari mpya la kifahari la Babu limeagizwa kutoka Japan

No comments: