Wednesday 29 May 2013

LAWAMA ZOTE KWA CLOUDS KUHUSU KIFO CHA NGWEAR



Mtayarishaji wa Muziki wa Bongo Fleva Prof Ludigo alieshirikiana na P Funk Majani kutengeneza Wimbo wa Mikasi wa Marehemu Albert Mangwear ametoa lawama kwa Radio ya watu Clouds Fm kuwa uongozi wake ndio umekuwa chanzo kikuu kusababisha kifo cha Msanii Mangwea aliefariki kwa kutumia madawa ya Kulevya.

Prof Ludigo katika ujumbe wake aliomtumia P funk akimtaka ampe Taarifa Mmiliki wa Radio Hiyo Kusaga Kuwa hataki kusikia wimbo wa Mikasi Ukichezwa katika Radio hiyo kwa kudai kuwa wao ndio wamemtumia vibaya msanii huyo na kumfanya aingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya kama njia moja wapo wa kupunguza mawazo aliokuwa nayo mpaka umauti umemkuta jana.

Ludigo amesema kuwa hakufanya jambo lolote enzi za Uhai wa msanii huyo kwa sababu alihofia gharama za kuishi mjini kwa msanii huyo aliekuwa akitumiwa na watu hao katika kazi mbalimbali.

No comments: