Friday 12 April 2013

SINTA AMEFUNGUKA JUU YA RAYUU

Baada ya muigizaji wa filamu na video model Alice Bagenzi AKA Rayuu kupiga picha za kuonyesha tattoo zake, mtangazaji wa kipindi cha Harusini cha DTV, Sinta, ambaye inaonekana hakupenda kitendo hicho, kutokana na picha hizo kuwa za “utata” amemchana Rayuu kwenye website yake, sintah.com.

“Hivi mtasema mimi namuonea kuandika hivi ama?? mimi ni mtambo wa kurekebisha tabia kwakweli waigizaji wengine wanatafuta umaarufu kwa kasi sana,sasa huyu so called msanii wa Bongo wa filamu anataka atoke,na ameshatoka sasa,una pose upigwe picha ili watu wakuone ktk mitandao ili iweje? kama sio kutaka umaarufu kunuka,” ameandika Sinta.
“Rayuu or whatever u call ya self wewe ni msichana mzuri kwanini unakimbizana na umaarufu ?waacha umaarufu ukufuate sio wewe uu kimbize ndio maana watu wanawachukulia cheap kwasababu ya matendo yenu ya kukurupuka na upungufu wa mawazo. You wanna be rihhana sio? shame on you!!!!!!!!!!!!!!!!!!”
Rayuu, ambaye ameigiza kwenye filamu kama The Image, Trinita Show, Sound of Death, One House n.k, amefunguka na kutoa kauli yake kuhusu alichosema Sintah. Kwenye ukurasa wake wa facebook, Rayuu ameandika:
“Sintah dn talk on tings ambazo hujui zilipo anzia u were supposed to ask coz u dn evn knw wea da pic came from besides kwan mgongo ni uchi or tatoo ni uchi i may nat speak may b bcz i dn c da reason ya mm kupoteza pumzi yangu on smthng ambacho kimesababishwa na mtu mmoja and kwann usinge nifata personal if u really want to correct me!pics za uchi mnaziacha hiyo tatoo imekuwa gumzo! Having tattoos on ma body s nat a crime anyway!na pia mgongo c uchi!”
“B4 Kumsafisha mwenzako make sure upo msafi na ww!!” Aliongeza. (picha/screenshot chini)
Rayuu akionyesha tattoo zake. Picha via dartalk.com Rayuu akionyesha tattoo zake
Rayuu Sintah

No comments: