Wednesday, 12 February 2014

TISHIO BONGO MOVIE KUTOKA DODOMA (DANIEL BAZA) WAKONGWE WATETEMEKA

 Daniel baza msanii kutoka dodoma atangaza vita kwa wasanii wakubwa wote wakae vizuri kwan yeye amekuja kuleta mapinduzi katika game, msanii huyo baada ya maongezi marefu na mwandishi wetu Noddy jr alimwambia haogopi mtu na kwenye game hana masihala
 msanii huyoa alietamba vilivyo na kazi kama chozi la zina ambayo inasambazwa na watever films amesema amejianga vilivyo na kazi zake zainazokuja. wasanii wakongwe baada ya taarifa hio wastuka na kujipnga vilivyo. DANIEL BAZA amesema hana hofu na kazi za wasanii wakubwa kwani wanaonekana kuishiwa idea na kurudia rudia kwenye kazi zao. '' Naona kazi nyingi za hawa wasanii walio tutangulia kuishiwa idea na kurudia rudia mara shikamoo mzee, mara naenda kwa mzee ni heri wafanye vitu vya tofauti ngojeni muone vitu ninavyo vipika mimi kwa sasa vipo jikoni mda si mrefu vitatoka''
msanii huyo anaonekana kujiamini sana kwa kazi zake zijazo na nyingine BONGO MOVIES STAR WAKE UP DANIEL BAZA IS COMING WITH HIGH SPEED.
SOURCE; noddy jr

MICHELLE OBAMA ASIMAMA KAMA MZAZI NA KUTOA USHAURI KWA WAZAZI WA JUSTINE BIEBIER

                      
Justin Bieber ni msanii ambaye amekuwa katika vichwa vingi vya habari miezi kadhaa ya karibuni, sio kwasababu ya kazi nzuri anayoifanya bali ni kutokana na vurugu na uvunjaji wa sheria wa kupita kiasi, kiasi kwamba hivi karibuni wananchi wa Marekani wamempigia kura (Deport Bieber Petition) ya kuiomba serikali imrudishe kwao sababu wamechoshwa na tabia zake.


Mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama ametoa ushauri kwa wazazi wa msanii huyo, akijitolea mfano kama yeye ndio angekuwa mzazi wa Bieber (19), kwa kueleza kile ambacho angejaribu kufanya kumsaidia mwanaye katika kipindi hiki ambacho ameonekana kuwa na changamoto nyingi zinazoonekana kusababishwa na umri wake (foolish age).
First Lady amesema kama yeye angekuwa mzazi wa Bieber angejaribu kuwa naye karibu muda wote, na kuzungumza naye na kumshauri.
“Mimi ningekuwa karibu naye sana kwenye maisha yake katika kipindi hiki….kuongea naye, ili kujua nini kinaendelea katika kichwa chake, na kujua nani yuko katika maisha yake na nani hayuko.” Alisema Michelle katika mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha Univision Radio.
Kuna uwezekano ushauri wa first lady ni siri ya mafanikio ya malezi bora wanayoyapata mabinti zake wawili Sasha na Malia, ambao pamoja kuwa ni watoto wa Rais wa taifa kubwa duniani lakini wanaonekana kuwa na nidhamu.
”[Kids] just want you near, you know — they want that advice from a parent. They want to see you on a daily basis, because the thing is he’s still a kid. He’s still growing up. So, I would pull him close.” Aliongeza Michelle.


Credit:Bongo5.com

TANGAZO LA KUUZA NYUMBA ZA MFUKO WA PSPF


                 Mfuko wa Pensheni wa PSPF unapenda kuutaarifu Umma kuwa umezindua Mpango Mpya wa uuzaji nyumba zake zilizojengwa kwa ajili ya makazi katika mikoa ya Dar es Salaam- Ilala (Buyuni), Morogoro (Lukobe), Tabora (Usule), Mtwara (Mang’amba), Shinyanga (Ibadakuli) na Iringa (Mawelewele).

Bei za nyumba ni kati ya sh. 52,000,000.00 hadi sh. 71,000,000.00 (bila VAT). Bei hizi ni kulingana na ukubwa wa nyumba na mkoa nyumba ilipo.   Ukubwa wa nyumba ni kuanzia vyumba viwili hadi vinne.

Chini ya utaratibu huu mpya unaoanza kutumika kuanzia Februari 2014; Muombaji atapaswa kuainisha kwenye fomu ya maombi aina ya nyumba anayohitaji na Mkoa ilipo.  Malipo yanaweza kufanyika kwa njia zifuatazo:

1)                           UNUNUZI KAMA MPANGAJI (HIRE PURCHASE):

Mnunuzi atalipia kwa mpango wa mwezi mmoja mmoja au miezi mitatu kwa mkupuo (installments) kulingana na thamani ya nyumba. Katika mpango huu, mnunuzi anaweza kulipia kutokana na vyanzo vingine vya mapato yake mbali na mshahara wake. Mwanachama wa PSPF aliyechangia chini ya  miaka mitano (5) atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 5,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba na asiye mwanachama wa PSPF atatakiwa kulipia kiasi cha sh. 10,000,000.00 kama malipo ya mwanzo ya nyumba kukidhi vigezo vya kununua nyumba (kama mpangaji).

Mpango huu wa Ununuzi kama Mpangaji (Hire Purchase) utamwezesha mnunuzi kulipa kati ya sh. 450, 000.00 (laki nne na hamsini tu) na sh. 813,000.00 (laki nane na kumi na tatu tu) kwa mwezi kama malipo ya nyumba zinazouzwa na Mfuko kulingana na ukubwa na eneo nyumba ilipo.

2)                           MALIPO YA MARA MOJA (OUTRIGHT PURCHASE)

Mnunuzi atalipia gharama ya kununua nyumba kupitia akaunti ya Mfuko na kisha kusaini makubaliano kabla ya kuhamishiwa umiliki (transfer).

3)                           MKOPO WA NYUMBA KUPITIA BENKI (MORTGAGE BASIS):

Mnunuzi anaweza kuchukua mkopo katika mojawapo ya Benki ambazo Mfuko wa PSPF ina mikataba nazo na kutumia mkopo huo kununulia nyumba. Mabenki hayo ni; CRDB, Azania, Exim na NMB. 

MUHIMU! Iwapo utanunua nyumba kupitia mkopo wa benki (Mortgage) utapaswa kuwa umesajiliwa kwenye Mfuko na kuchangia kwa muda wa miaka mitano au zaidi. Muda wa kurejesha mkopo ni mpaka miaka ishirini na mitano (25) kulingana na matakwa ya Benki husika.

Mwombaji anayehitaji kuona au kukagua nyumba awasiliane nasi kupitia simu: +255 22 2120912/52 au +25522 2127375-6 au E-mail: pspf@pspf-tz.org.

Kwa maelezo zaidi fika Makao Makuu ya PSPF yaliyopo jengo la Golden Jubilee Towers, Barabara ya Ohio au ofisi zetu zilizopo katika kila mkoa.

Imetolewa na
Mkurugenzi Mkuu,
Mfuko wa Pensheni wa PSPF 

PENZI MOTO MOTO RAY NA CHUCHU WAPI JOHARI SOMA HAPA


ISHAKUWA SHIDA.....PENZI LA RAY NA CHUCHU SI SIRI TENA...WENYEWE WAITANA VISURA:




Penzi kati la waigizaji wawili maarufu ndani ya bongo movie, Vicent Kigosi – Ray na Mwanadada Chuchu Hans limekuwa sio siri tena baada ya hivi majuzi mwanadada Chuchu hans kuweka picha mbalimbali za Vicent kigosi na yeye kwenye mtandao mmoja wa
kijamii huku akiandika “I love my babyface NO MATTER WHAT (TOO MUCH)” akimaanisha kuwa anampenda sana mwigizaji huyo  kwa hali yoyote ile na anampenda sana.

Penzi hilo limekuwa la utata baada ya kuleta mtafaruku hapo siku za awali baina ya waigizaji Johari na chuchu Hans kudaiwa kuzitwanga wakimgombania muigizaji huyo.
Source:Bongo Movies

Tuesday, 11 February 2014

MWINGIRA AGOMA KUPIMA UKIMWI, NADAI YA KUSALITI NDOA YAKE NA KUZAA NA MKE WA MTU

MWINGIRA AGOMA KUPIMA UKIMWI, MADAI YA KUZAA NA MKE WA MTU



Mtume na Nabii wa Kanisa la Efatha, Joseph Elias Mwingira. MTUME na Nabii wa Kanisa la Efatha, Joseph Elias Mwingira anayekabiliwa na kesi ya kuzaa na mke wa mtu, hatimaye amefunguka mengi kuhusu madai hayo lakini amekataa kabisa kupima Ukimwi, Risasi Mchanganyiko lina kila kitu.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili katika Mahakama ya Hakimu Mkazi - Kisutu, Dar, umebaini kuwa Mwingira aliye na kesi mahakamani hapo yenye namba 306 ya 2013, iliyofunguliwa na mlalamikaji Dk. Morris William, amejibu tuhuma zinazomkabili kwa njia ya maandishi.
Majibu hayo yameandaliwa na Kampuni ya Uwakili ya Legal Link, ambapo nakala yake imefikishwa kwa wakili wa mlalamikaji Dk. William, Januari 22, mwaka huu.
Pamoja na mambo mengine, madai yaliyopo katika jalada la kesi hiyo, mlalamikaji Dk. William, ameomba mahakama ikubali Nabii Mwingira apimwe Ukimwi na kipimo cha utambuzi wa vinasaba ‘DNA’.
Nabii huyo amepinga vikali ombi hilo, akieleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo (la madai ya kifedha).

MADAI YA MAPENZI
Katika majibu hayo (nakala tunayo), Mwingira amekanusha kufanya mapenzi na mlalamikiwa namba mbili, Dk. Phillis Nyambi ambaye ni mke wa mlalamikaji.
“Mlalamikiwa namba moja amefafanua kuwa hakuingia katika uhusiano wa kimapenzi na mlalamikiwa wa pili,” imeeleza kampuni inayomtetea Mwingira.

AKANA KUBAKA
Nabii huyo pia amekanusha madai ya kumbaka mlalamikiwa wa pili kama alivyosema mlalamikaji katika hati yake ya malalamiko iliyopo mahakamani hapo.
Nabii Mwingira pia amekana madai ya kuzaa na mlalamikiwa namba mbili na kuwepo kwa matatizo ya kitabibu kwa mama huyo ambaye sasa ana mtoto mwenye umri wa miaka mitano, akasema mlalamikaji anatakiwa kuthibitisha.

Kuhusu madai ya Dk. Phillis kushiriki kimapenzi na Mwingira hivyo kusaliti ndoa halali na kumharibia furaha ya maisha mlalamikaji, nabii huyo amesema hajawahi kuwa na uhusiano wowote wa kimapenzi na mwanamke huyo.
Kuhusu madai ya Mwingira kutembea na mke wa mlalamikaji na habari hizo kuandikwa magazetini na kwenye mitandao ya kijamii hivyo kumdhalilisha na kumshushia hadhi, amedai kuwa yeye hahusiki na hilo na atahitaji kuthibitisha.
Madai mengine ya mlalamikaji kwamba vitendo vya walalamikiwa namba moja na namba mbili vya kujihusisha kimapenzi vimemuathiri Dk. Morris kisaikolojia na kiuchumi na kumfanya apoteze biashara zake za kimataifa kwa kukosa wadhamini katika NGO yake, Mwingira amesema kama yametokea hakuyasababisha yeye.
Ameiomba mahakama kuitupilia mbali kesi hiyo na kumuamuru mlalamikaji kulipa gharama za kesi hiyo, hivyo ameweka pingamizi la awali.

Saturday, 21 September 2013

HAPPINESS WATIMANYWA AIBUKA KIDEDEA REDD'S MISS TANZANIA 2013.


Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kushoto ni mshindi wa tatu,Clara Bayo.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakifungua shindano la mwaka huu kwa kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano la mwaka huu ambalo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania.Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.

 Warembo walioingia hatua ya kumi na tano bora. 
 Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Dkt. Ramesh Shah akitangaza Warembo walioingia hatua ya tano bora.
Warembo walioingia hatua ya tano bora,toka shoto ni Happiness Watimanya,Elizabert Peter,Clara Bayo,Lucy Tomeka pamoja na Latifa Mohamed.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakipita jukwaani na mavazi ya aina mbali mbali wakati wa Onyesho la Taifa Redd's Miss Tanzania 2013 linalofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam usiku huu. 
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya hapa nchini,Lady Jay Dee akitoa burudani kwenye Onyesho la Redd's Miss Tanzania 2013,linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam. 

Thursday, 19 September 2013

RIPOTI YA KUHUSU KUACHIWA HURU KWA AGNES MASOGANGE NA MELISA HUKO AFRIKA KUSINI




WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa.
  
Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya.
  
Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8.
  
Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.
  
“Kusema kweli nguvu ya kesi ya akina Masogange imepungua sana mara baada ya kubainika aina ya dawa walizokuwa nazo. 

"Kama zingekuwa ni dawa za kulevya, mambo yangekuwa mengine lakini kwa haya waliyokamatwa nayo, sidhani kama kuna kesi ngumu sana. Nataraji watapewa dhamana wakati wowote kutoka sasa,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili ndani ya Jeshi la Polisi. 

Masogange na mwenzake wanashikiliwa nchini Afrika Kusini tangu Julai, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Sheria ya Dawa za Kulevya ibara ya 26 (1) a na b, dawa zinazotambulika kama za kulevya hapa nchini ni kama vile Cocaine, Heroin, Mandrax, Bangi, mirungi na nyingine lakini ephedrine haimo katika kundi la dawa za kulevya.
  
Ni sheria hiyo ambayo imetamka wazi kwamba mtu anayekamatwa na dawa hizo zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 haruhusiwi kupewa dhamana lakini zikipungua thamani hiyo, anaweza kupewa dhamana.
  
Vyanzo vya Raia Mwema vimebainisha kwamba kwa vile Ephedrine si dawa za kulevya kwa mujibu wa sheria zilizopo, watuhumiwa hao wanaweza kupewa dhamana.
  
Kwa mujibu wa mwongozo wa wadau wa mapambano dhidi ya Dawa ya Kulevya uliotolewa mwaka 2011, uingizwaji na matumizi ya dawa kama hizo zinazofahamika kwa jina la vibashirifu, unatawaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
  
Gazeti hili lilipiga hodi katika ofisi za TFDA jijini Dar es Salaam ambako lilielezwa kwamba vibashirifu huingizwa nchini kwa utaratibu maalumu kulingana na mahitaji ya kitaifa yaliyopo.
  
“Unapozungumzia vibashirifu, unazungumzia mambo ya kitaalamu. Nitakupa mfano, kuna mmea unaitwa Coca. Mmea huu unatengeneza dawa za kulevya zinazofahamika kwa jina la cocaine lakini ni mmea huo huo ndiyo unatengeneza soda ya Cocacola ambayo karibu kila mtu anatumia.

“Mtu anaweza kutumia Ephedrine kutibu magonjwa kama vile mafua lakini anaweza kuitumia pia kama dawa za kulevya. Unajua baadhi ya dawa zilizo kwenye kundi la dawa za kulevya zinatumika pia hadi kwenye hospitali mbalimbali lakini kwa shughuli na kiwango maalumu.
  
“Mtu akitaka kuagiza dawa hizo ni lazima apate kibali kutoka kwetu. Tukizikamata kwa mtu ambaye hana kibali tunaziteketeza. 

Hiyo ndiyo adhabu ya kwanza lakini kama kutaonekana kulikuwapo na nia ya uhalifu, basi mkono wa sheria utachukua mkondo wake, alisema mmoja wa maofisa waandamizi wa TFDA aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji rasmi wa mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, matumizi ya Ephedrine yalianza nchini China miaka zaidi ya 200 Kabla ya Kristo na inapatikana sana katika mmea wa Ma Huang ambao unatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika tiba za Kichina.
  
Mwaka 1994, aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Argentina, Diego Maradona, aliondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini Marekani na baadaye kufungiwa kucheza soka baada ya kukutwa na hatia ya kutumia Ephedrine ambayo ni miongoni mwa dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
  
Raia Mwema limekosa taarifa za kwa nini vyombo vyote vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kwamba dawa walizokutwa nazo zilikuwa ni Methamphetamine lakini sasa taarifa mpya zinataja kuwa ni Ephedrine.

Hata hivyo, nyaraka tofauti ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kwamba Ephedrine na Methamphetamine zinafanana kila kitu tangu kwenye muundo wa molekyuli (chembe) zake isipokuwa Ephedrine ina kitu kinachoitwa Hydroxil ambacho hakipo kwenye Methamphetamine.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa hizi mpya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema anafahamu kuhusu hilo lakini wao wanaendelea na upelelezi wao kuhusu watu waliowatuma akina dada hao kupeleka dawa hizo nchini Afrika Kusini.
  
“Haya mambo yanafanyika huko Afrika Kusini na sisi hatuwezi kuingilia labda kama wakitaka kitu kutoka kwetu. Cha msingi kwetu ni kwamba dawa hizo zilitoka kwetu na wasichana wale hawana uwezo wa kuwa na mzigo wenye thamani ile. 

Tunawatafuta wahusika na tukipata taarifa tutawapa,” alisema Nzowa ambaye anatajwa kujijengea heshima kubwa kwenye vita hii dhidi ya dawa ya kulevya. 

Source:Raia Mwema

Tuesday, 3 September 2013

CHADEMA WAMKANA AFANDE SELE....WADAI HAWAJAWAHI MUOMBA AGOMBEE UBUNGE MOROGORO


Gazeti la Habari Leo la siku ya leo tarehe 2 Septemba lenye kichwa cha habari "Chadema kuzoa wasanii mastaa" pamoja na mambo mengine, mwandishi amemnukuu mmoja wa wasanii toka mkoa wa Morogoro akisema amewahi kuombwa na viongozi wa mkoa wa CHADEMA kugombea Ubunge. 

NAOMBA KUWEKA KUMBUKUMBU SAHIHI.
1. Mimi ndiye mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Morogoro, ninayeongoza Baraza la Uongoz la mkoa lenye wajumbe wa5 tu tangu mwaka 2009. 
2. Katika vikao vyetu vyote hukujawahi kuwepo kwa AGENDA ya kumuomba/ kumshawishi mtu yeyote kugombea nafasi yoyote. 
3. Hatujawahi kumuomba Afande Sele kugombea. Mbali na hilo hatujawahi hata kumuomba tu kujiunga na CHADEMA.  
  4. Kwa upande wa gazeti la Habari leo, naungana na kauli ya JB kwamba, kuna dalili za wazi kwamba habari hii imepikwa na mwandishi mwenyewe. 

Asanteni Makamanda.
PUUZENI TAARIFA HII Susan Limbweni Kiwanga

DIAMOND NA LINAH SANGA NDANI YA MAPOZI YA UTATA KWA MARA NYINGINE TENA


Tabia mbaya! Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya

Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani

Shushushu wetu aliwapiga chabo ‘wakifanya yao’ hadi Diamond alipokwenda stejini na kuangusha bonge la shoo huku akimwacha Linah mpweke.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.



Mwanahabari wetu alipomuuliza Linah kuhusu ishu hiyo, alifunguka: “Weweee…hakuna ni mapozi tu na wala usiandike hiyo habari.”
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao kabaya wanakaendekeza.

SOURCE: GPL

CHUPI NA SHANGA ZA MSANII SHILOLE ZAANIKWA NJE- FIESTA

Dance imekolea kwa shilole hapo ...mpaka mambo yote hadharani ......kitu cha black

HIVI WEMA ALIMKOSEA NINI DIAMOND, KAMPIGA TENA KIJEMBE KWENYE WIMBO WAKE MPYA

Leo video ya muziki ya Msanii Diamond platnumz ya wimbo wa My Number one imetoka rasmi kwenye Television na mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema ukweli ni moja ya video nzuri sana za muziki hapa nchini na sio siri kijana huyu wa bongofleva amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi.

Baada ya kuisikiliza kwa makini nyimbo hii yenye mahadhi flani ya kiafrika zaidi tulifika kwenye dakika ya 2 na sekunde 50 (2:50) ya nyimbo hii na ndipo ukatokea “ubishi” ambao tukaona sio mbaya tukiupeleka kwa wasomaji wetu ili kupata maoni Zaidi.

Katika sehemu hii ya mwisho ya nyimbo hii Diamond anatamka maneno ambayo baadhi ya watu tuliokuwepo katika mabishano hayo tunasema kuwa yanamlenga mwanadada wetu muigizaji, Wema sepetu kama “vijembe” kwakwe, diamond anamalizia wimbo wake kwa kusema “TUACHE TULALE” maneno amabyo kwa wale wanafuatilia habari za watu hawa wawili yalioongewa na mpenzi wa diamond wa sasa VJ penny kwenye tukio la wapenzi hao kumrekodi mwanadada Wema Sepetu kwenye simu alipokuwa akimbembeleza mpenzi wake wa zamani (Diamond Platnumz) warudiane, tukio liliotokea miezi kadhaa iliyopita.

Swali likawa, Je maneno haya yatakuwa yanamlenga Wema??? Kama siyo kwanini Diamond ayatamke sehemu ambayo hata haihusiani nayo kwenye wimbo???

Tuesday, 27 August 2013

DEMU MKENYA AFUNGUKA UHUSIANO WAKE NA DIAMOND PLATINU


Demu Mkenya Angel Maggy, aliyedaiwa kutoka na Staa wa Bongo Fleva Nasib Abdul‘Diamond Platinum’ambaye ni mtangazaji wa kipindi cha Tujuane cha kituo cha Tv cha KTN cha nchini humo amefunguka na TEENTZ kuhusiana na uhusiano wake na msanii huyo wa Bongo


Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Jijini Nairobi alisema kuwa hana uhusiano na msanii huyo na anashangaa hayo maneno kusambaa na kwamba yeye ni shabiki mkubwa wa Diamond.
‘No …Diamond is apal lyk any other..yy shld I date him??Am not in love with him’alisema Angel.
Alipoulizwa kwanini ameamua kuchora tattoo ya msanii huyo kwenye mkono wake alisema kuwa kuchora…


Jast tat I got atattoo named diamond doesn’nt mean ama dating him’alisema Angel.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari za burudani vya Kenya, zilisema kuwa ishu ya kutoka na Diamond ilianza kuvuma mara baada ya kufanya shoo mbili katika Miji ya Nairobi na Mombasa nchini humo,ambapo aliporejea Bongo ndipo ukaibuka mlipuko wa habari zilizomhusu na mrembo huyo.


Jast tat I got atattoo named diamond doesn’nt mean ama dating him’alisema Angel.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari za burudani vya Kenya, zilisema kuwa ishu ya kutoka na Diamond ilianza kuvuma mara baada ya kufanya shoo mbili katika Miji ya Nairobi na Mombasa nchini humo,ambapo aliporejea Bongo ndipo ukaibuka mlipuko wa habari zilizomhusu na mrembo huyo.

Ilisemekana kuwa alipokuwa akifanya shoo kwenye Ukumbi wa KICC, Nairobi siku ya kwanza, Diamond aliimba wimbo wake wa Ukimuona maalum (dedication) kwa ajili ya Angel, jambo lililomfanya mrembo huyo kuonekana ‘spesho’ miongoni mwa maelfu waliohudhuria onesho hilo.

Imeripotiwa kuwa baada ya shoo hiyo kumalizika USIKU, Angel alionekana ‘beneti’ na Diamond wakielekea katika hoteli aliyofikia staa huyo Nairobi.

DIAMOND AHOJI... "MIMI NAONA NI SAAWIA KABISA........AU WEWE UNASEMAJE"....???

Kwenye Mapenzi kuna mengi ya kupitia,mapenzi ni
kama maisha ya kila siku,kuna kupata na kukosa
lakini ukijaaliwa uzima unaendelea kupigana hadi
mwisho cha msingi kuto kukata tamaa...


Kwenye mapenzi yakubidi uwe mvumilivu,mwenye
 mapenzi ya kweli na muaminifu ili kulinda
penzi la dhati toka kwa mwenzi wako pindi
unapokuwa kwenye dimbwi la mapenzi....
Ikitokea bahati mbaya siku ukamfumania mpenzi
wako na Kisha ukaweza kumsamehe Basi wewe
ndiye my #Number One........Binafsi kigezo hiko
 naweza tumia mimi binafsi kama Naseeb Abdul
Juma,maswali nakuachia wewe
mtu wangu wa kweli Je wewe ukimfumania mpenzi
wako waweza msamehe na kuendelea
kuwa na mahusiano kati yenu wawili......??
Msamaha utakaokutoka ni kweli ni
wa dhati toka moyoni......?? Mi nimemaliza
nahitaji sikia vigezo vyako kumjua number one wako..
.

MCHAWI AANGUKA AKIWA KWENYE HARAKATI ZA KULOGA


Mchawi hivi karibuni kaleta kizaa zaa huko Dzivarasekwa  alipokutwa na 'birthday suit' yake(uchi)

 Sabina Rokuzhe alikiri kuwa yeye ni mchawi na amedondoka alipokuwa anaruka kwenye ungo akitokea kwenye trip yake ya kuloga huko Masvingo.


Alikutwa kwenye nyumba ya Mbuya Annah Kamupaundi. AkaaAnza kuwaomba watu waliomzunguka wasimpige ,akasema pia katembelea nyumba kadhaa katika eneo hilo.


Mmoja wao aliyemuona asubuhi mapema ni Mrs Alice Hundi (37) ambae alisema aliamka baada ya kusikia mayowe ya mwanamke kwenye saa nane hivi usiku.


"Nilipomuona yuko uchi,nilimmwagia  chumvi usoni, akaanguka na kuanza kujizungusha zungusha chini. Tuliita polisi na akachukuliwa"


Polisi walitoa uhakika kwamba amechukuliwa na atapewa msaada wa psychiatric.

Sunday, 18 August 2013

FEZA KESSY MATITI YOTE NJE NJE UZINDUZI WA VIDEO MPYA YA LADY JAY DEE






Video ya yahala ilizinduliwa rasmi jana pande za nyumbani lounge. Baadhi ya wasanii kama Feza Kessy ambaye alikuwa mgeni rasmi, Vanessa Mdee  na  Mkolon...

Pamoja  na  kuwa  mgeni  rasmi, Feza  anadaiwa  kuwa  miongoni  mwa  wasanii  waliokuwa  wamevaa  vibaya huku sehemu kubwa ya matiti yakiwa wazi

Vazi   lake  lilikuwa  likiyaanika  matiti  yake  hadharani, hali  ambayo  iliwafanya  hata  watoto  wayashuhudie.

Saturday, 17 August 2013

POLISI FEKI AJITETEA......ADAI KUWA NJAA NDO ILIMFANYA AJIFANYE TRAFFIC.......


MKANDA mzima wa askari bandia wa Kikosi cha Usalama Barabarani (trafiki), James Juma Hussein (45)  aliyekamatwa saa 1:30 asubuhi ya Agosti, 14, 2013 maeneo ya Tabata Kinyerezi Mnara wa Voda, jijini Dar es Salaam akiwa ndani ya sare zake za kazi, umepatikana....
  
Kwa nini James alikamatwa? Asubuhi hiyo, afisa mmoja wa trafiki mwenye cheo cha ukaguzi alikuwa akipita eneo hilo kwenda kazini, alipomwona James alisimamisha gari, akashuka kwenda kumsalimia. 


Lakini alishangaa kuviona vifungo vya shati lake ni vya kawaida (vya polisi vinatakiwa kuandikwa police force yaani ‘jeshi la polisi’), akamtilia shaka. 

Afisa huyo Alimkamata ‘askari feki’ huyo  mkazi wa Kimara Matangini, Dar na kumfikisha kwenye Kituo cha Polisi Stakishari, wilayani Ilala, Dar akafunguliwa jalada namba STK/RB/15305/2013 KUJIFANYA ASKARI ili taratibu za kisheria zichukuliwe juu yake.

Ndani ya kituo cha polisi, James alihojiwa haya: Askari: Wewe mtu wa wapi?
James: Mnyamwezi wa Tabora.
Askari: Una muda gani ukijifanya trafiki?
 James: Wiki moja sasa.
Askari: Hii kofia ya polisi uliipata wapi?
James: Nguo nyeupe juu ya kofia niliitengeneza kienyeji, krauni, tepe za usajenti na mkanda ni za shemeji yangu alikuwa polisi Tabora, ni marehemu, alikuwa akiitwa Shaban.

James aliwaambia polisi kuwa suruali nyeupe ya kitrafiki aliishona mtaani lakini kamba ya filimbi na kizibao cha kung’ara vilikuwa vya polisi.

Askari: Uliwahi kuwa polisi?
James: Niliwahi kupata mafunzo ya upolisi katika Chuo cha Polisi Moshi (CCP) mwaka 1990-91 lakini nilifukuzwa kazi kwa sababu nilikwenda muziki. Nilirudi Tabora nikawa mkulima na mke wangu na mtoto mmoja ambao wote sasa ni marehemu.

Ndani ya nguo za kitrafiki alizokuwa amevaa James, alikutwa na suruali ya bluu na fulana ya kijani.

James alisema njaa ndiyo iliyomfanya ajifanye trafiki na ‘kuwapiga mikono’ madereva, hasa wa daladala ili anapowakuta na makosa kwenye magari yao ajipatie chochote.


 Kamishina wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Suleiman Kova amethibitisha kukamatwa kwa polisi huyo feki

AJIFUNGUA KOBE BAADA YA MIEZI 10 YA UJAUZITO...............



A tradomedical practitioner in Lagos has claimed that a 20-year old woman delivered a tortoise and a baby girl in his clinic. The woman, Rasheedat Raimi, said she had carried the pregnancy for 10 months before she eventually delivered the baby girl and the tortoise at a trado-medical clinic on Mutairu Street, Off Ijegun Road, outskirts of Lagos. She was in pains as she talked to P.M.NEWS about the strange delivery. “I came to Yakafi for prayers because of the terrible pains I was having in my stomach. Immediately I got here, prayers were offered and immediately there was a burst of water and blood under me.
 The tortoise came out with the placenta and the baby came out later. I couldn’t believe my eyes, but I was very weak. I was happy the pain left me. I felt relieved after the delivery. Ithank God,” she told P.M.NEWS slowly. On whether she attended ante-natal clinic before the delivery, the young woman said: “I carried the pregnancy for 10 months. I did scans several timesand nobody told me that I was carrying tortoisein my womb. What they alwaystold me was that I am alright and would deliver at the right time,” she added. “This is amazing, but true. She did not register with my clinic for ante-natal. When she came here with her people, she was in pains, we didn’t know she will deliver here

Friday, 16 August 2013

Lulu kama Diamond Platnumz, kuzindua Foolish Age mlimani City, soma hapa


Lulu kama Diamond Platnumz, kuzindua Foolish Age mlimani City, soma hapa
Hatimaye mwanadada Elizabeth Michael (Lulu) yupo teyari kuachia filamu yake ya kwanza toka atoke jela, filamu aliyoipa jina la Foolish age inayotarajiwa kuzinduliwa rasmi tarehe 30 mwezi huu.
Akiandika kwenye ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii leo mchana lulu aliandika.
“Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu....!!!ninafuraha ya kuwafahamisha kuwa TAREHE 30/8/2013 ndio siku nitakayozindua movie ya mpya ya FOOLISH AGE....hatimaye narudi kazini!!!!Uzinduzi utafanyika katika ukumbi wa MLIMANI CITY....kutakuwepo na wasanii mbalimbali wa muziki....na pia LADY JAY DEE pamoja na MACHOZI BAND atakuwepo pia!!!nahitaji support ya mashabiki wote wa LULU na mashabiki wa BONGO MOVIE.....
Filamu hii inasambazwa ka kampuni ya PROINPROMOTERS.
Huu utakuwa ni uzinduzi mkubwa wa filamu nchini baada ya msanii wa upande wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platnumz kufanya shoo kubwa ya mziki kwenye ukumbi mkubwa na maarufu wa mlimani city jambo ambalo sio la kawaida kwa wasanii wa filamu na muziki hapa nchini.

Mtoto wa Riyama ageuka kuwa kero kwa waongozaji wa filamu


Mtoto wa Riyama ageuka kuwa kero kwa waongozaji wa filamu
Mtoto wa kike wa mwigizaji Riyama aliyejifungua hivi karibuni amegeuka kuwa kero wa waongozaji wa Filamu wa nchini kutokana na mwanadada huyo kwenda naye kwenye kila location anapotengeneza Filamu hivyo kusababisha usumbufu katika utengenezaji wa Filamu GPL wameripoti.
Akizungumza na gazeti la ijumaa mmoja wa waongozaji wa Filamu alisema kuwa mwanadada Riyama asipoangalia anaweza kupotea kisanii kwani kila unapotaka kumchezesha kwenye Filamu lazima umuandalie chumba cha kulala yeye na familia yake kutokana na mtoto wake mdogo huyo.
Habari inasema kuwa eti, mwanadada Riyama hawezi kwenda kulala mwenyewe na kumuacha bwana wake huyo, sasa baadhi ya wasanii wanamkwepa kitu ambacho kitamuathiri.
Naye Riyama Akizungumzia hilo alisema: “Kulala chumba kimoja na wasanii wenzangu ni kitu nisichokipenda. Ndiyo maana huwa napenda niwe na chumba changu mimi na baba mtoto wangu, mwanangu na dada wa kazi, kama mtu hataki basi siwezi kucheza filamu yake.”

WALTER CHILAMBO AFUNGUKA BAADA YA NEY WA MITEGO KUSEMA ANAMAISHA DUNI..LICHA YA USHINDI WA MIL 50



Baada ya maneno na tuhuma nzito za Ney wa Mitego dhidi ya Mshindi wa Epiq Bongo Star Search mwaka 2012, Walter Chilambo kuwa 'huenda' amedhulumiwa zawadi yake ya ushindi, Shilingi Milioni 50 na waratibu wa shindano hilo kwa sababu mpaka sasa yupo katika maisha duni, Msanii huyu amevunja ukimya na kusema kuwa yeye yupo vizuri tu.
Walter amesema kuwa maneno haya hayana ukweli wowote na yeye anaishi vizuri tu na kwa Ney, Hadhani kama alikaa chini na kufikiria kabla ya kuongea kuhusiana na issue hii katika wimbo wake, wala hakufanya uchunguzi wowote ambao uliomhusisha yeye.
Walter amesema kuwa yeye na Ney hawana ukaribu wowote, na walishawahi kukutana hivi karibuni na alipomuuliza ni kwanini amemuimba vile katika wimbo wake, Ney alimwambia kuwa 'asipanik' then akapotezea na mambo issue nyingine na kisha kutimua zake.
Walter amemaliza kwa kusema kuwa, Maneno haya hayamuumizi vile hayana ukweli wowote, na vilevile hayawezi kumuondolea mashabiki wake.

MWAKYEMBE AWATAJA WANAOHISIKA NA KUPITISHA WENYE MADAWA AIRPORT, SOMA HAPA.





Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akiongea na waandishi wa habari leo ofisini kwake jijini Dares salaam juu ya hatua zilizochukuliwa na Wizara ya Uchukuzi juu ya sakata la madawa ya kulevya yaliyokamatwa huko Afrika Kusini hivi karibuni.Dkt. Mwakyembe amewafukuza kazi mtandao mzima uliohusika kusaidia kusafirisha madawa hayo, pia Waziri Mwakyembe ameliagiza jeshi la Polisi kuwakamata wafanyakazi hao na kuwaunganisha na wenzao kujibu mashitaka ya jinai.




Waziri wa Uchukuzi,Mh.Dkt. Harison Mwakyembe akionyesha picha ya Msanii Agness Gelard maarufu kwa jina la Masogange mbele ya waandishi wa habari,masogange alikamatwa na madawa ya kulevya huko nchini Afrika Kusini hivi karibuni
.



waandishi wa habari wakimsikiliza kwa makini Waziri wa Uchukuzi akiwa anafafanua hatua zilizochukuliwa na Serikali kuushughulikia mtandao mzima uliosaidia kupitisha madawa ya kulevya

Saturday, 10 August 2013

BAADA YA COCA COLA KUMLETA DIAMOND NA NDEGE BINAFSI KUTOKA KENYA HIKI NDIO AMEFIKIA KUKIFANYA



Ukimpigia simu na Diamond Platnumz na isipokelewe, usimind sana, sababu hafanyi makusudi, anakimbizana na schedule za kupiga hela tu.

Baada ya jana Cocacola kumchukulia private jet toka Nairobi hadi Dar es Salaam, Bongo Flava Prince, Nasib ameingia mzigoni kushoot tangazo jipya la Cocacola. Kwenye picha za utengenezaji wa tangazo hilo alizoziweka kwenye Instagram, Diamond anaonekana akitembea huku akinywa soda hiyo.


Source:Bongo5