Monday, 6 May 2013

Ruge mutahaba atoa amri kwa wafanyakazi wake..Hakuna kupiga bongo fleva leo..


Kasema hivyo baada yakuzungumzia ishu ya Jide na Clouds na kusema ina maamuzi yake na mfano ni leo hakuna kupiga nyimbo za Bongo Flava, kwamba Clouds ina maamuzi binafsi Kwasababu ni redio binafsi so kutopiga nyimbo za Jide ni maamuzi pia...Pia ameongelea kuwa kinacho mfanya lady jay dee Awashutumu ni maswala binafsi tu ikiwemo Band ya Skylight inayomilikiwa na mtangazaji wa Clouds FM kupata umaarufu mkubwa kwa sasa kuliko Band yake ya Machozi Band...So kumfanya Lady Jay Dee kuweweseka,.

Sunday, 5 May 2013

Tukio la Mlipuko wa Bomu katika Ufunguzi wa kanisa la St. Joseph Parokia ya Olasiti Arusha

Tukio la Mlipuko wa Bomu katika Ufunguzi wa kanisa la St. Joseph Parokia ya Olasiti Arusha

Kwa sasa hali ya kawaida inaanza kurudi. Vyombo vya usalama vinaendelea kuchunguza ili kujua mlipuko huo ni nini hasa.
Balozi wa papa nchini na viongozi wa juu wa jimbo wameondoka eneo la tukio salama na balozi hajadhurika kabisa ingawa mlipuko huo ulilipuka karibu nao.
Mkuu wa mkoa alikuja na sasa ameondoka.
Wananchi wameanza kupungua eneo la tukio na wengi wanaelekea Mount Meru ili kuwatambua majeruhi. Hivyo idadi ya watu wanaondoka eneo la tukio na kwenda hospitali.
Polisi wamekamata pikipiki ambayo inasadikiwa imetumika katika tukio hilo.
Shughuli ya uzinduzi wa kanisa hilo imeahirishwa hadi tarehe ambayo haijatajwa
Mungu awajalie majeruhi wapate nafuu haraka.

Mwingira wa EFATHA Awaita Viongozi wa Serikali ni Washenzi

Mwingira wa EFATHA Awaita Viongozi wa Serikali ni Washenzi

Leo Wakati Mwingira anatoa mahubiri yake
 kanisani. Anadai ameonyeshwa serikali wamemtuma mtu aje hapa kanisani ku spy ndipo alipoanza wewe uliyetumwa ni mshenzi na mambo yako ni yakishenzi sababu waliokutuma ni washenzi, Swali nalojiuliza Kwanini Mwingira Anakuwa na Hofu na watu wa serekali..Je kuna kitu anakificha? Wacha serekali ifanye kazi yake na si kuwatukana

Kwanini Raila anaweweseka na kifo cha mzee Mutula kilonzo

Kwanini Raila anaweweseka na kifo cha mzee Mutula kilonzo

A Kenyan journalist in UK has reported that former Prime Minister Raila Odinga on monday met the private anthropologist hired by Mutula kilonzo family at a London hotel before the doctor left for Kenya.

Though the details of the meeting were not disclosed.... the meeting indicated a wider conspiracy to cover the actual cause of the Makueni Senator or even try and frame the Govt of mistrust and murder


Je Raila anahusika katika mpango mzima wa kumlwakatare mzee Kilonzo????!!

Maswali mengi kuliko majibu lakini yote yanaweza kuwa majibu,tusubiri.

Gadner Afunguka Kuhusu Beef la Mke Wake Lady Jay Dee na Clouds FM

Gadner Afunguka Kuhusu Beef la Mke Wake Lady Jay Dee na Clouds FM


Leo nilipata nafasi ya kuzingumza na Gadan G Habash ambaye ni Meneja na Mume wa Mwanamuziki maarufu nchin Lady Jay Dee, sote tunafahamu juu ya maneno aliyoyasema Lady Jay Dee kama ni Wosia wake.
Kupitia kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm haya ndio yalikuwa majibu ya maswali niliyomuuliza Gada G;
Ipi ni Kauli yako juu ya Wosia wa Lady Jay Dee...?

Gadna G: Ni maneno  ambayo yametoka moyoni mwake na  ni maneno  mbayo anajitetea kama msanii,  mimi kama Meneja ukiacha pia kama  mke wangu naendelea kumsapot kwa kile ambacho anaona ni sawa, basi mimi nitaendelea kumsaport  na kujaribu kuzungumza na Lady Jay Dee, mara nyingi anasema tu kwamba  watu wasifikilie ni swala la wimbo kupigwa au kutokupigwa, hayo ni mambo ya kawaida lakini wafikirie tu kwamba huyu mtu anaongea kutokana experience yake aliyokuwa nayo na wale watu.
Baada ya mwaka 2003 kuacha kufanya kazi kwenye management yao ya Smooth Vibe, yalitokea mambo mengi hapa katikati  ila hakusema lakini siku za hivi siku za karibuni kuna mengine ambayo yametokea, ndio akaona hapana nisipo sema nitazidi kukandamizwa na matokeo yake nitakufa kisabuni.

Hii ni kama vita mmejipangaje..?

Gadna G: Unapoamua kusema ukweli swala la kujipanga mara mbili huwa halipo, ni kwamba unasema ukweli watu wasikie  naukizungumzia uhasama watu watauliza juu ya uhasama  lakini ulikuwepo tayari kwahiyo tu watu wanajua kwa sasa kwa kuwa jdee ameamuwa kuongea lakini tu hawajui tu kwamba jdee alikuwa na matatizo na wale watu tangu kipindi cha nyuma sababu wale watu wanafumo dume ya kufanya kazi na alipoachananao aliona kama wanamfatilia  kulekule ambapo yeye alipo

Nini mlikiona kama chokochoko...?

Gadna G: Unajua kwa mfano unaweza kumuomba mtu maji akakwambia sina, ukayaona yale  pale ukamwambia niuzie akakuuzia ila bado alivyokuuzia  akaona kama unafaidi, mwisho  akakwambia yameisha nenda sehemu nyingine, ukaenda sehemu nyingine na ukayapata bure, akaona umepata akaamua kukufata kulekule na akakukuta unakunywa maji kwenye grasi kisha akakuputa, sasa hapo inabidi useme hapa unavyofanya sio sawa ndo hicho anachofanya Jay Dee sasa hivi.

Hali hii imewaathiri kwa kiasi gani...?

Gadna G: Cha kushukuru Mungu ni  kwamba msanii au hata pia stesheni ya redio inategamea umma wa Watanzania au  hata mashabiki kwa ujumla kwa kuwepo kwake.
Jay Dee anapata saport nzuri kutoka  Watanzania, basi ujue hata hajaathirika chochote, na pia tu anaendelea kufanya kazi kwa bidii, ila tu isipokuwa unapoona mtu anafanya madhara ili tu mtu apate athari fulani ndio unasimama kuongea, ndiyo maana tuna Bunge na watu wanasimama, watu wanaongea, watu wanatetea hoja, ndiyo maana yake. Yani lazima mtu usimame useme ukweli kwa unalohisi hili jambo litanipa madhara nisiposema.

Kwa Wasanii wengine unawaambiaje...?

Gadna G: Uwoga ni kitu ambacho binadamu tumeumbiwa, wakati mwingine unasaidia wakati mwingine unakudhiru uwoga wako,kwa sababu wanasema adui wa maendeleo yako mwenyewe ni wewe mwenyewe, ndiyo maana uwoga wako unaeza ukasabishwa ukakandamizwa zaidi, ndiyo maana wazee wetu waliweza kusimama na kuikomboa hii nchi kwa sababu walisimama hawakuogopa. Wangeogopa hii leo hii nchi tusingekuwa huru, kwa hiyo kama kuna mtu ana jambo na anaogopa kusema hilo ni jambo la kawaida kuogopa, lakini wakati wa kusema ukifika usiogope kusema ili mradi useme ukweli, basi inatosha....

Kauli yako ya mwisho ni ipi..?

Gadna G: Ni kwamba wanahitaji kujua ukweli na kuambiwa ukweli, mtu yoyote anayejua kitu cha kweli  anaweza kusema sio sawa, utaendelea kukandamizwa. Kauli ya mwisho  ndo hiyo wanahitaji kuambiwa ukweli na  kusikia ukweli  ili kama wanakosea wasiendelee kukosea  wabadilikee….

Mwisho..!
AKIONGEA NA  MTANGAZAJI DAN CHIBO MTANGAZAJI WA TBC FM,NA HIVI NDIVYO ILIVYOKUWA

Mbunge Nassari Akitoa Damu Kuwapa Majeruhi wa Mlipuko wa Bomu Arusha


Nassari Akitoa damu kwa Majeruhi  Mlipuko wa Bomu
Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari mbali ya kuwahamasisha watu kutoa damu, pia hivi punde amemaliza kutoa damu kwa ajili ya kuwachangia majeruhi waliolipukiwa na bomu kanisani LEO. Pichani Nassari akionekana akitoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na Mbunge wa Arumeru Mashariki, Jushua Nassari LEO tangu majira ya saa 5:30 asubuhi wamekuwa wakifanya kazi ya kuwahamasisha watu kutoa damu kwa ajili ya kuwawekea majeruhi mbalimbali waliojeruhiwa na bomu katika kanisa la Parokia Mpya ya Olasiti mjini humo.

Kutokana watu wengi kupoteza damu na kumwagika kwa wingi. Mbali na hilo baadhi ya wahudumu wa hospitali hiyo wameueleza mtandao wa Habarimasai.com kwamba hivi sasa wana wakati mgumu katika kufanya usafi na mwandishi wetu Joseph Pantaleo ameshuhudia manesi hao wakisafisha damu sakafuni kila wakati huku wakimwaga maji na dawa ili kuondoa mabaki ya damu hiyo.

Lema na Nassari wameonekana wakiwahamisisha watu kutoa damu na wengi wameitikia wito huo. Endelea kusoma habarimasai.com kwa taarifa mbalimbali zaidi

Breaking Newzzzz....MLIPUKO MKUBWA UNAO SADIKIKA KUWA NI BOMU WATOKEA KANISANI OLA CITY ARUSHA ASUBUHI HII

1:42 AM    No comments

MLIPUKO MKUBWA UNAO SADIKIKA KUWA NI BOMU  WATOKEA KANISANI  OLA CITY ARUSHA  ASUBUHI HII.PICHA  NA TUKIO ZIMA KWA UNDANI UTAVIPATA HIVI PUNDE ENDELEA KUTEMBELEA MTANDAO HUU

I'm listening to Sijaona Kama Wewefullsong.mp3 @Hulkshare:

I'm listening to Sijaona Kama Wewefullsong.mp3 @Hulkshare:

Saturday, 4 May 2013

vitambulisho halali vya wafanyakazi wa blog yetu




Ghasia zaendelea mjini Conakry, Guinea

 4 Mei, 2013 - Saa 14:49 GMT

Watu kama watatu wameuwawa nchini Guinea katika mapambano baina ya polisi na waandamanaji waliodai uchaguzi huru na wa haki.
Maandamano ya mwezi March mjini Conakry
Ghasia zimekuwa zikiendelea kwa siku ya pili katika mji mkuu, Conakry.
Afisa mmoja wa upinzani alieleza kuwa waliokufa walikuwa wafuasi wa upinzani.
Upinzani nchini Guinea unasema Rais Alpha Conde hakuwashauri kabla ya kutangaza siku ya uchaguzi wa wabunge kuwa tarehe 30 Juni.
Upinzani unataka wafuasi wake wafanye maandamano hadi rais afute uchaguzi huo.
Rais Conde alishika madaraka mwaka wa 2010 baada ya uchaguzi wa kwanza wa kidemokrasia tangu mwaka 1958.
Lakini uchaguzi wa wabunge uliopangwa kufanywa mwaka wa 2011 umekuwa ukiahirishwa kwa sababu wanasiasa wameshindwa kuwafikiana.

Wahisani waahidi dola bilioni 3.6 kwa Darfur


 9 Aprili, 2013 - Saa 10:54 GMT
Hali ya njaa katika Darfur
Nchi wafadhili wa Darfur, wameahidi kutoa dola bilioni 3.6,za maendeleo na ukarabati wa jimbo la Darfur, kuweza kutolewa kwa kipindi cha zaidi ya miaka sita ijayo.
Tangazo hilo limetolewa wakati wa kilele cha kongamano la kimataifa la siku mbili kuhusu Darfur nchini Qatar ilikuwa mwenyeji.

Taarifa zinazohusiana

Waandalizi walitaka kuchangisha dola bilioni 7.2 za mpango wa maendeleo ambayo inalenga kuliweka jimbo hilo katika hali ya kujitegemea.
Takriban watu 300,000, wanaaminika kufariki wakati wa vita vya mwongo mmoja, katika jimbo la Darfur, kulingana na takwimu za Umoja wa Mataifa.

Wengine milioni 1.4 wanasalia kuwa wakimbizi.

Wakosoaji wanasema kuwa juhudi za kuleta amani katika jimbo hilo, zimehujumiwa kwani migogoro na migawanyiko haiishi katika jimbo hilo.
Maandamano yanayopinga kongamano hilo yalifanyika Darfur siku ya Ijumaa .
Wanaharakati wanasema kuwa maandamano yaliitishwa kwa sababu ukosefu wa usalama ulihujumu shughuli za ukarabati.
Pia wanasema kuwa wanapinga mkataba wa amani ulioafikiwa mwaka 2011 ambao ulitiwa saini nchini Qatar lakini ukakataliwa na makundi ya wapiganaji.
Hata hivyo, rasimu ya mkakati wa maendeleo, uliochapishwa kabla ya kuanza kwa mkutano, ulisema kuwa kucheleweshwa kwa shughuli hiyo utatatiza ukarabati.
Mgogoro katika jimbo la Darfur ulianza mwaka 2003 wakati waasi walipoanza kushambulia maslahi ya serikali na kutuhumu serikali ya Rais Bashir kwa kuwakandamiza waarabu weusi.
Kundi la wapiganaji wa kiarabu la Janjaweed lilituhumiwa kwa kuwaua waarabu weusi katika jimbo la Darfur
Ingawa ghasia katika jimbo hilo zimepungua, bado kuna makabiliano kati ya serikali na wanajeshi wa serikali, wapiganaji, wezi wa mifugo na makundi hasimu ya kikabila.
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir, anatakikana na mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita kwa mauaji ya kimbare katika jimbo hilo.

Mashambulizi ya makombora Sudan

 8 Oktoba, 2012 - Saa 16:27 GMT

Milima ya Nuba , Kordofan Kusini

Watu watano wameuawa na wengine 23 kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na waasi katika jimbo la Kordofan Kusini, kwa mujibu wa taarifa za redio ya taifa.
Mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa, alisema kuwa makombora matano yalirushwa ndani na nje ya mji mkuu wa Kordofan Kusini, Kadugli,hali iliyosababisha wafanyakazi wa kutoa misaada kukimbilia usalama wao katika maeneo ya wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa.
Waasi hao wamekiri kufanya mashambulizi hayo ingawa walikana kama raia walijeruhiwa.
Waasi wamekuwa wakipigana katika jimbo la Kordofan Kusini, karibu na mpaka wa Sudan Kusini , tangu mwaka jana lakini mji wa Kadugli umekuwa tulivu kwa miezi kadhaa kabla ya kuanza tena kwa vurugu hizo.
Sudan Kusini ambayo ilijitenga na Sudan mwaka jana, imekana madai ya kuunga mkono waasi hao.
Redio ya taifa, Radio Omdurman, haikusema ikiwa majeruhi walikuwa raia au wanajeshi.
Awali, jeshi la Sudan, lililaumu waasi wa SPLM-North, kwa mashambulizi hayo.
Msemaji wa jeshi la Sudan, alielezea kuwa waasi wa SPLM-North walijaribu kuingia ndani ya mji wa Kadugli na kushambulia eneo lenye umbali wa kilomita sita, Mashariki mwa Kadugli.
Umoja wa mataifa ulisema kuwa wafanyakazi wake wa misaada waliondolewa katika eneo hilo na kupelekewa katika kambi ya jeshi kama hatua ya tahadhari.
Mfanyakazi mwingine wa umoja huo alidokeza kuwa mashambulizi yalianza nyakati za asubuhi, akiongeza kuwa makombora mawili yalianguka katika makao ya shirika la UNICEF ingawa hayakulipuka.
Mapigano katika jimbo la Kordofan Kusini, yamekuwa mojawapo ya maswala nyeti ambayo yamekuwa yakichochea hali ya taharuki kati ya Sudan na Sudan Kusini katika mwaka mmoja uliopita.

Tanzania yafuta matokeo kidato cha Nne


 3 Mei, 2013 - Saa 18:28 GMT
Miongoni mwa wanafunzi wakifurahi baada ya matokea ya mtihani
Serikali ya Tanzania, imeagiza mitihani yote ya kidato cha nne kwa mwaka 2012, kusahihishwa upya baada ya Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, Mizengo Pinda ya kuchunguza sababu zilizosababisha matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 kuwa mabaya, kuwahi kutokea katika historia ya mitihani nchini humo.
Asilimia 60 ya watahiniwa walianguka mitihani hiyo na kusababisha serikali kuunda tume ya uchunguzi baada ya wadau wa elimu, wazazi na wanafunzi kulalamikia matokeo hayo.
Tume hiyo ilichunguza sababu zilizosabisha matokeo ya kidato cha nne mwaka 2012 kuwa mabaya, na imependekeza kwa serikali kufuta matokeo yote ya mitihani hiyo na isahihishwe upya.
Uamuzi huo umetangazwa katika kikao cha Bunge la Tanzania linaloendelea na vikao vyake mjini Dodoma na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera na Uratibu, William Lukuvi.
Tume hiyo, ilipewa hadidu za rejea kadhaa ikiwemo kutafuta sababu za matokeo mabaya ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012; Kubaini sababu za kushuka kwa kiwango cha ufaulu katika mitihani ya Kidato cha Nne mwaka 2011 hadi 2012; Kutoa mapendekezo ya hatua za kuchukua kukabiliana na tatizo la mwenendo wa kushuka kwa kiwango cha elimu mara moja,kipindi cha muda mfupi, kati na kipindi cha muda mrefu. Pia Tume hiyo ilipewa jukumu la kutathmini nafasi ya Halmashauri katika kusimamia Elimu ya Sekondari katika Halmashauri zake; na kuanisha sababu nyingine zinazoweza kuwa zimechangia hali hii ya matokeo.
Uchambuzi wa taarifa hiyo ya awali unaonyesha kuwa kutokana na uchunguzi uliofanyika, kwa muhtasari, Tume imebaini mambo muhimu kadhaa kama vile matokeo ya Kidato cha Nne kuanzia mwaka 2008 kuendelea kushuka kuliko miaka iliyotangulia kwa sababu mbalimbali ikiwemo changamoto zinazotokana na mafanikio yaliyopo sasa ya kuongezeka sana kwa Idadi ya Shule za Msingi na za Sekondari,hasa kati ya mwaka 2001 na 2013; na hivyo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo Shuleni.Kwa mfano, katika kipindi cha mwaka 1961 hadi 2001 Idadi ya Wanafunzi wa Shule za Msingi imeongezeka kutoka Wanafunzi 486,470(1961) hadi 4,875,764 mwaka 2001, sawa na ongezeko la Wanafunzi 4,389,294
katika kipindi hicho cha takriban miaka 40.
Hata hivyo, ongezeko hilo haliendani na mazingira ya kufundishia na kujifunzia, ikiwemo upungufu wa miundombinu muhimu ya shule kama vile madarasa,maabara, madawati, maktaba, nyumba za walimu, hosteli na majengo mengine muhimu ya shule. Vilevile, kuna tatizo la uhaba wa walimu,vitabu, zana za kufundishia na matatizo ya ukaguzi wa shule.
Tume imebaini pia kwamba, pamoja na Wanafunzi hawa kuwa katika mazingira yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita na kwamba ufanisi katika shule kwa ujumla umekuwa unashuka kwa sababu mbalimbali,zikiwemo za mabadiliko ya mchakato wa kuandaa na kutoa matokeo ya mtihani kwa mwaka 2012. Mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.
Hata hivyo baadhi ya wadau wa elimu, wazazi na wanafunzi wamehoji uamuzi huo wa serikali kama hautakuwa na athari kwa wanafunzi waliofaulu na kujiandaa na masomo ya kidato cha tano na wale ambao tayari wamejiandikisha kurudia mitihani yao kwa njia ya kulipia.

Kazi za uokozi zasimamishwa Darfur


 4 Mei, 2013 - Saa 13:53 GMT
Kazi za uokozi zilizokuwa zikifanywa Darfur, Sudan, kutafuta wafanyakazi 100 walionasa kwenye mgodi wa dhahabu ulioporomoka Jumatatu zimesimamishwa.
Darfur
Walioshuhudia tukio hilo wanasema msako katika mgodi wa Jebel Amir umesimamishwa kwa sababu ni hatari kuendelea na kazi za uokozi.
Hapo jana waokozi tisa piya walinasa kwenye mgodi huo.
Hakuna aliyenusurika.
Inaarifiwa kuwa migodi midogo-midogo ya Sudan ilitoa dhahabu ya thamani ya zaidi ya dola bilioni-mbili mwaka jana.
Madini hayo yanaipatia Sudan sarafu za kigeni ambazo zilipungua sana baada ya Sudan Kusini kujitenga mwaka wa 2011 na kubaki na visima vingi vya mafuta.

Monday, 29 April 2013

Uwanja wa Ndani wa FBF kukamilika Juni

Uwanja wa Ndani wa FBF kukamilika Juni

Child Soldiers Used by Central African Republic Rebels



Elephant Poaching on the Rise
Picture1.png
By Shawn Humphrey | Yahoo! Contributor Network – Fri, Apr 26, 2013
Children are the subject of widespread human rights violations by the Seleka rebel coalition in the Central African Republic (CAR), the United Nations News Service reported on Thursday.
Among the allegations by a senior U.N. official are reports are killings, sexual violence, and the use of child soldiers in the Seleka rebellion against CAR. Additionally, there are reports that elephants in the protected Dzanga-Sangha area are increasingly being poached, according to the Associated Press.
Here's a closer look at the report and the crisis in CAR.
Armed and uniformed children seen on military duties
Leila Zerrougui, the Secretary-General's Special Representative for Children and Armed Conflict, said that uniformed and armed boys had been seen at checkpoints and participating in looting in every town controlled by the Seleka coalition. "I call on all military commanders in charge of the different armed groups in the Séléka coalition to immediately release children within their ranks and to issue command orders to refrain from further recruitment and use of children," she said, according to the U.N. News Center.
In addition, cases of rape and sexual violence against girls has been reported to the U.N., and 2 million children are in need of humanitarian assistance due to the ongoing violence in the country.
Bombardment of residential areas killed 29 children in one week of the crisis.
Poaching increases in protected region
The World Wildlife Federation's head of anti-poaching policy, Bas Huijbregts, said that "elephant poaching is on the increase and given the fact that Central African Republic for the moment is also in dire straits we are fearing for the worst in terms of people trying to look seriously for ivory," according to the AP.
Huijbregts attributed the lawlessness to the increased poaching, which saw 40 elephants killed after rebels overthrew the government. However, the WWF says it isn't possible to know how many elephants have died due to a lack of forest patrols.
The rainforest preserve is in the southwestern region of the country, where 3,400 forest elephants live.
A report from Reuters indicated that eight conservation groups were meeting in Brazzaville, Republic of the Congo, to try to find ways to curb the poaching epidemic. Poaching of elephants is fueled by a demand in Asia for ivory which has killed an estimated 20,000 to 30,000 elephants in Africa per year.
Shawn Humphrey is a former contributor to The Flint Journal and an amateur Africanist, focusing his personal studies on human rights and political issues on the continent.




."