TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Jeshi la Polisi nchini, linapenda kuufahamisha umma kuwa, mnamo tarehe
15/02/2014 siku ya Jumamosi katika viwanja vya Polisi Barracks, barabara
ya Kilwa, jijini Dar es Salaam, kutakuwa na hafla ya kumuaga IGP
Mstaafu Said Alli Mwema kuanzia saa mbili asubuhi hadi saa sita mchana.
Ikumbukwe kuwa, katika kipidi chake cha uongozi wa Jeshi la Polisi, IGP
Mstaafu Said Alli Mwema alishirikiana vyema na wananchi wa kada zote
wakiwemo wadau mbalimbali wa amani, hususani katika dhana ya Ulinzi
shirikishi na Polisi Jamii. Jeshi la Polisi nchini kwa kulitambua hilo,
linatumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wote kuhudhulia hafla hiyo.
Aidha, IGP Mstaafu Said Alli Mwema katika uongozi wake alianzisha na kusimamia mifumo mbalimbali ya kuzuia na kukabiliana na uhalifu hapa nchini ikiwemo maboresho ndani ya Jeshi la Polisi, ili kuhakikisha Jeshi linafanya kazi kwa weledi, usasa na ushirikiano na wananchi.
Imetolewa na:
Advera Senso-SSP
Msemaji wa Jeshi la Polisi.
No comments:
Post a Comment