Wednesday, 12 February 2014

BAADA YA AJALI MBAYA YA NDEGE... ALGERIA YATANGAZA SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO

Ndege aina ya Hercules C-130 baada ya kupata ajali
Algeria imeanza siku tatu za maombolezi ya kitaifa kufuatia ajali ya ndege iliyowaua watu 77 Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Abiria mmoja alinusurika ajali hiyo iliyohusisha ndege aina ya Hercules C-130 iliyoanguka katika eneo la milima ya Oum al-Bouaghi, ikiwa njiani kuelekea mji wa Constantine.


Kikosi cha uokoaji kikiwa eneo la tukio.
Ripoti zinasema hali mbaya ya anga ilisababisha ajali hiyo ya ndege.Wengi wa abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo ni maofisa wa kijeshi na familia zao.

Mwanajeshi aliyenusurika, anaripotiwa kuendelea kupokea matibabu katika hospitali moja mjini Constantine baada ya kupata majeraha ya  kichwa.

Wizara ya Ulinzi imesema kuwa imeunda tume maalum kuchunguza ajali hiyo na kuwa Ahmed Gaid Salah, ambaye ni mkuu wa majeshi na Naibu Waziri wa Ulinzi atazuru eneo la ajali hiyo.
>>gpl

No comments: