![](http://2.bp.blogspot.com/-_InVjII8Z3k/UvuAmohdAJI/AAAAAAAAr8Y/qiy3nGKrb4I/s400/nem.jpg)
TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI
UCHAGUZI MDOGO WA UBUNGE JIMBO LA KALENGA
Tume ya Tifa ya Uchaguzi imepokea barua kutoka kwa Mhe. Spika wa
BUNGE la Jamhuri ya Muungano Tanzania ya kuiarifu uwepo wa nafasi wazi
ya Ubunge katika Jimbo la Kalenga lililopo katika Halmashauri ya Wilaya
ya Iringa Vijijini, kufuatia kifo cha Mbunge wa Jimbo hilo Mhe. William
Mgimwa aliyefariki dunia tarehe 1/1/2014. Baada ya taarifa hiyo Tume
imepanga ratiba ya Uchaguzi mdogo katika Jimbo la Kalenga kama ifuatafyo:-
- Uteuzi wa Wagombea Ubugne utafanyika tarehe 18-Februari-2014
- Kampeni za Uchaguzi zitaanza tarehe 19-Februari-2014 hadi 15-Machi-2014
- Siku ya kupiga kura ni Jumapili terehe 15-Machi-2014
Wagombea wanatakiwa kuwasilisha Fomu za Uteuzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi
wa JImbo la Kalenga siku ya Uteuzi si zaidi ya Saa 10:00 Alasiri. Tume
inawataarifu Wananchi wote pamoja na Vyama vya Siasa kufuata ratiba
iliyotolewa pamoja na kushiriki katika mchakato mzima wa Uchaguzi
kuanzia siku ya Uteuzi hadi siku ya Kupiga Kura ili watimize haki yao ya
Kikatiba ya Kuchagua viongozi wanaowataka.
Tume inawasisitiza wananchi wote katika maeneo husika kujitokeza kukagua tarifa zao wakati wa kuweka wazi Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili kuona kama kuna marekebisho madogo yanahitajika kufanyika kuwawezesha kupiga Kura bila malalamiko yoyote. Ikumbukwe kwamba hakutakuwa na uandikishaji mpya wa Wapiga Kura.
J. Mallaba
MKURUGENZI WA UCHAGUZI
No comments:
Post a Comment