MKURUGENZI wa Kampuni ya Filamu ya Endless Fame, Wema Sepetu hivi karibuni amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya majirani zake kumshitaki kwenye serikali ya mtaa kufuatia tabia ya wafanyakazi wake kutiririsha maji machafu mtaani.Taarifa iliyolifikia gazeti hili inadai kuwa, majirani wa Wema katika eneo analoishi, Kijitonyama jijini Dar wamekuwa wakimlalamikia msanii huyo kwa kitendo hicho lakini imeonekana uvumilivu umewashinda. “Mara kwa mara wafanyakazi wake wamekuwa wakitiririsha maji hapa mtaani sasa leo tumeona tukamshitaki serikali za mitaa ili sheria ichukue mkondo wake,” alisema mmoja wa majirani wa staa huyo aliyeomba jina lake lisiandikwe gazetini.Juni 26, mwaka huu Ijumaa lilifika kwenye nyumbani kwa Wema na kushuhudia maji yakitoka kisha kuzagaa mtaani na muda mfupi baadaye alifika Afisa Mtendaji wa Kata ya Makumbusho (jina halikufahamika mara moja) ambaye aligonga kwenye nyumba ya Wema, baada ya muda alitoka binti wa kazi aitwaye Bite.
Katika mazungumzo yao,
Bite alionekana kujitetea lakini baadaye ilibainika wana makosa na
akatakiwa kwenda ofisi za kata kwa maelezo zaidi. Amri hiyo
ilionekana kuwa ngumu kwa Bite na wafanyakazi wenzake ambapo busara
zilitumika na kiongozi huyo wa serikali akataka walipe faini na kuwaonya
waache tabia hiyo.
|
Saturday, 29 June 2013
WEMA KUBURUZWA MAHAKAMANI KWA KUTIRIRISHA MAJI MACHAFU MTAANI...!!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment