MSANII wa filamu na muziki Bongo, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ ametoa kali
ya mwaka baada ya kunaswa akiingia ‘supermarket’ akiwa ametinga taulo
Tukio hilo lilitokea hivi karibuni katika mji wa Maryland nchini
Marekani ambapo staa huyo amekwenda kwa ajili ya kufanya shoo kisha
kupigwa picha hiyo na rafiki yake ambaye aliiweka mtandaoni ikimuonesha
akiwa amefunga taulo kwenye matiti.
Paparazi wetu alipomuuliza Shilole kulikoni kupitia mtandao wa Instagram, alifunguka:
“Huku
watu wanaishi kizungu hakuna mtu anayeshughulika na maisha ya mwenzake
kila mmoja anahangaika na mambo yake kwa hiyo siyo ajabu mimi kuvaa
taulo na kwenda nalo supermarket, huku ni kawaida tu.”
No comments:
Post a Comment