
LORI la mafuta limeanguka jioni hii katika eneo la milima ya sekenke mkoani Singida na kuua watu wanne papohapo.
Chanzo cha
ajali hiyo ni kufeli breki lori hilo kukamata moto wakati lilipokuwa
linashuka milima hiyo. Shuhuda wa ajali hiyo, bwana Julius Chacha
alipoongea na Dj Sek Blog amesema kuwa lori hilo lilipoacha njia
lilipinduka na kuingia bondeni na kushika moto.
Akiendelea
kuongea, shuhuda huyo alisema walishindwa kutoa msaada wowote kwa kuwa
moto uliposhika ulikuwa mkubwa na hawakuwa na vifaa vya kuokolea. Watu
wanne wamekufa papohapo kutokana na ajali hiyo. Polisi walikuwa bado
hawajafika eneo la tukio mpaka tunaondoka eneo la tukio.

Wanainchi wakiangalia Lori baada ya kuungua

Mabaki ya Lori hilo bada ya kuteketea kabisa na moto jioni hii

Baadhi ya wasafiri wakitazama lori lililongua jioni hii


Bonde la mlima sekenke linavyoonekana na baadhi ya miti imeunguaa


Haya ni mabaki ya mwili wa mmoja ya watu walikuwam kwenye Lori hiloo

(Picha na DJ Sek Blog)
No comments:
Post a Comment