Thursday, 20 February 2014

FACEBOOK YASEMA ITAINUNUA WHATSAPP ILI KUONGEZA THAMANI YAKE



 
Kampuni ya mtandao wa Kijamii ya Facebook imesema kuwa itanunua mtandao wa mawasiliano ya ujumbe mfupi wa WhatsApp kwa kima cha dola bilioni 16, na nyongeza zaidi ya dola bilioni 3 zitakazolipwa waanzilishi wa mtandao huo pamoja na wafanyikazi wake.
 
Hiyo ndiyo biashara kubwa zaidi ya ununuzi kuwahi kutekelezwa na Facebook hadi kufikia sasa.
 
WhatsApp ni maarufu sana miongoni mwa vijana wanaotafuta kuepuka kulipia huduma ya kutuma ujumbe mfupi wa simu yaani SMS. WhatsAp imeweza kuwasajili zaidi ya watumiaji milioni 450.
 
Katika taarifa, mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg amesema kuwa mtandao huo upo njiani kuwaunganisha watu bilioni moja jambo  ambalo  litaifanya Facebook kuwa na thamani kubwa.

No comments: