Yanga wakifurahia mojawapo ya magoli kutoka katika mechi hiyo. Picha kwa hisani ya Bin Zubeiry Blog
Timu ya soka ya Yanga, jioni hii imewadhihirishia mashabiki wao na
wapenzi wa soka barani Afrika kwamba msimu huu ulikuwa wao baada ya
kuwachapa wapinzani wao wa jadi,Simba kwa jumla ya magoli 2-0 katika
mchezo wa mwisho wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mchezo ambao
ulionyeshwa kote barani Afrika kupitia SuperSport East 9 ndani ya DStv.
Mashabiki wa soka nchini Tanzania na
barani Afrika waliweza kuona mpambano huu wa watani wa jadi Live kupitia
kwenye luninga zao kwenye SuperSport 9 East ambao walirusha matangazo
hayo moja kwa moja kutokea Uwanja wa Taifa.
Katika mchezo huo magoli ya Yanga yalifungwa na Didier Kavumbagu
kunako dakika ya 5 ya kipindi cha kwanza na Hamis “Diego” Kiiza kunako
dakika ya 63 ya kipindi cha pili.Kwa matokeo hayo, Yanga inamaliza msimu wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 60, ikifuatiwa na Azam FC yenye 52 na Simba 45.Hii ni mara ya 24 kwa Yanga kutwaa taji la Ubingwa wa Soka Tanzania Bara. Hongera kwa Yanga!
No comments:
Post a Comment