Dodoma.
Bunge la Muungano linaendelea na vikao vyake leo mjini Dodoma baada ya
mapumziko ya siku moja, huku kukiwa na mabadiliko ya ratiba.
Katika mabadiliko hayo, hotuba ya Wizara ya Elimu imeondolewa kama ilivyotarajiwa na sasa italetwa bungeni Juni 3.
Taarifa
zinaeleza kuwa, kusogezwa kwa hotuba hiyo kunatokana na mipango ya
Serikali ambayo inatafuta namna na kukamilisha mchakato wa matokeo ya
kidato cha nne ili kuipa mteremko hotuba ya Waziri wa Elimu, Shukuru
Kawambwa (pichani) bungeni.
Tofauti
na mapumziko ya siku mbili za kawaida kwa wabunge, safari hii
walipumzika siku moja baada ya Jumamosi kutumiwa kwa ajili ya
kuhitimisha hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya
Nishati na Madini ambayo iliahirishwa Alhamisi iliyopita kutokana na
vurugu za Mtwara.
Ratiba
ya awali inaonyesha kuwa leo Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
ilikuwa isome hotuba yake ikifuatiwa na Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi kabla ya kuhitimisha wiki kwa kusoma Makadirio ya Wizara ya Mambo
ya Nje.
Wizara
ya Elimu ilikuwa katika ‘mtihani’ kwenye Kikao cha 10 cha Bunge mapema
Februari, hasa baada ya Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia kuwasilisha
hoja binafsi kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu na zaidi ni
kukosekana kwa mitalaa ya elimu.
Hatua
hiyo ililazimisha Waziri wa Elimu, Shukuru Kawambwa kupewa muda
kuwasilisha mtalaa huo na alifanya hivyo Februari 6, ukihusisha elimu ya
chekechea, elimu ya msingi na sekondari kabla ya kupitishwa na Bunge.
Kamati
ndogo iliundwa chini ya Magreth Sitta akiwemo Mbatia na wabunge wengine
waliobobea katika masuala ya elimu kuangalia uhalali wake.
Hata
hivyo, katika kile kinachoelezwa kuwa ni wasiwasi kwa Serikali kuhusu
hofu ya vivuli vya wabunge wa upinzani, ratiba ilibadilishwa na
kuisogeza mbele hotuba ya Wizara ya Elimu.
Ratiba
mpya ya Bunge sasa inaonyesha kuwa, leo Bunge litapokea hotuba ya
Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi ambayo itajadiliwa kwa siku mbili.
Hotuba
hiyo pia haitegemei kuwa na mteremko kwani wabunge watakuwa na shauku
ya kujadili kuhusu migogoro ya mipaka pamoja na masuala ya upimaji wa
ardhi ili kuondoa kero za wakulima na wafugaji yakiwemo mashamba
yanayomilikiwa bila kuendelezwa.
Baada
ya hotuba hiyo yatafuata Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Wizara ya
Kazi na Ajira na kufuatiwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Nchi kabla ya
kuhitimishwa kwa Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ambazo zote
zitakuwa zikisomwa na kujadiliwa kwa siku moja.
No comments:
Post a Comment