Taarifa
ya habari ya Star tv ya saa mbili usiku ya tarehe 23/11/2012 imeeleza
kuwa wanafunzi wa kike katika chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wanadaiwa
kufanya biashara ya ukahaba katika maeneo mbalimbali ya starehe mjini
Dodoma!
Habari
hii inasikitisha hasa ukizingatia umuhimu wa wasomi hawa katika
Tanzania na hatari inayoweza kuwapata kama taarifa hii ina ukweli.
Kama
jamii tujiulize, tatizo ni nini mpaka mtu wa level kama hiyo kuamua
kuvaa vichupi na kujiuza kwenye clubs na sehemu zingine??
CHUO
KIKUU cha Dodoma UDOM kinadaiwa kukumbwa na kashfa ya ngono kufuatia
madai kwamba baadhi ya wananafunzi wa kike wanajihusisha na biashara ya
kuuza miili yao kwa lengo la kujikimu kimaisha.
Tuhuma
hizo zimebainika wakati wa mahafali ya tatu ya UDOM huku takribani
wahitimu 6392 wakitunukiwa vyeti,stashahada,shahada za kwanza,uzamili na
shahada za uzamivu.
Chuo Kikuu
cha
Dodoma ambacho kilianzishwa rasmi mwezi machi mwaka 2007 kimejipatia
sifa kemkekm za kitaaluma licha ya ukweli kwamba bado ni kigeni machoni
pa wengi.
Tuhuma
za ngono miongoni mwa wanafunzi wa kike zinadaiwa kusababishwa na ukata
hatua inayowalazimu kutoroka chuoni nyakati za usiku na kujiunga na
baadhi ya wasichana wa mitaani waliokubuhu kwenye ukahaba maarufu kama
machangudoa kwa lengo la kujiuza.
Wakizungumza
na star tv wakati wa mahafali hayo baadhi ya wahitimu wanathibitisha
uwepo wa vitendo hivyo vilivyo kinyume na maadili.
Kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo Makamu Mkuu wa Chuo hicho Prof.Idris Kikula anatoa onyo kali kwa wote watakaobainika.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Dodoma Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amenukuliwa kwa
nyakati tofauti akisisitiza suala la maadili chuoni hapo hatua
inayodaiwa kupuuzwa na wanaojihusisha na vitendo hivyo.
IMETOKA KWA DJ SEK BLOG
No comments:
Post a Comment