SWEET HOME:Mourinho arudi rasmi Chelsea
maurinho
Posted Mei4 2013 saa 16:28 PM
In Summary
“Huwa si jambo la kawaida kuona mtu akisema ataondoka kwenye klabu fulani wakati hajakamilisha mipango.”
Habari zinasema kocha huyo wa Real Madrid
alikutana na mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich na kupata chakula cha
usiku kwenye mgahawa wa La Famiglia jijini London ambapo walifanya
mazungumzo ya kina na kocha huyo alikubali kutua Chelsea kwa dau hilo.
Hata hivyo kocha huyo atatakiwa kuweka mambo sawa
kati yake na uongozi wa Real Madrid kwa kuwa bado ana mkataba kwenye
klabu hiyo unaomalizika baada ya miaka mitatu.
Habari zinasema Abramovich atatakiwa kutoa kiasi cha pauni 12 milioni kwa Real Madrid ikiwa ni gharama ya kuvunja mkataba wa kocha huyo.
Habari zinasema Abramovich atatakiwa kutoa kiasi cha pauni 12 milioni kwa Real Madrid ikiwa ni gharama ya kuvunja mkataba wa kocha huyo.
Chelsea itamtambulisha kocha huyo kabla ya kuanza
kwa ziara za mechi za kirafiki, hiyo inamaanisha kuwa mechi ya kwanza ya
kocha huyo itakuwa dhidi ya Singha All Stars XI huko Thailand, Julai
17.
Msaidizi wa zamani wa Mourinho, Andre Villas-Boas, alisema anaamini kocha huyo ameshasaini mkataba mpya.
Kocha huyo wa Tottenham, ambaye aliwahi kufanya
kazi kwenye klabu alizopitia Mourinho, Porto na Chelsea alisema: “Nina
uhakika uamuzi wa mwisho umeshafanyika. Nadhani anafurahi kurudi
England, ni kama nyumbani kwake.
“Huwa si jambo la kawaida kuona mtu akisema ataondoka kwenye klabu fulani wakati hajakamilisha mipango.”
Villas-Boas aliongeza: “Ana historia nzuri kwenye
ligi hii, nadhani atatoa changamoto baada ya kuwasili hapa. Wachezaji
wanampenda na wamekuwa wakitaja jina lake mara kwa mara.”
Akiwa Chelsea, Mourinho alipata ubingwa wa Ligi
Kuu England msimu wa 2004/2005 na 2005/2006 pia alipata Kombe la FA
msimu wa 2006/2007. Alipata vikombe vya ligi msimu wa 2004/2005,
2006/2007 na Ngao ya Hisani, 2005.
No comments:
Post a Comment