Sunday, 12 May 2013

MNIGERIA AKAMATWA UWANJA WA NDEGE (KIA) NA UNGA


Vyombo vya ulinzi na usalama Uwanja katika wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (Kia), vimemtia mbaroni raia wa Nigeria akiwa amebeba kilo saba za dawa zinazoaminika ni za kulevya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alisema raia huyo wa Nigeria alikamatwa saa 8:00 usiku wa kuamkia juzi, akijiandaa kuingia katika jengo la uwanja huo.
Boaz alisema mtuhumiwa huyo ambaye amejitambulisha kuwa ni mfanyabiashara, alikuwa asafiri kwenda Ouagadougou kupitia Adiss Ababa kwa ndege ya Shirika la Ethiopian Airline.

No comments: