Yanga
imepinga mpango wa TFF kubadili ratiba ili michezo yake ionyeshwe
katika kituo cha Supersport. Kupitia kwa makamu mwenyekiti wa klabu
Clement Sanga, Yanga wamesema mpango huo unawatia hasara kwa kuwa
watatakiwa kucheza michezo mitatu ndani ya siku 8 badala ya mechi 2. Pia
wamesema uonyeshwaji wa michezo hiyo utapunguza mahudhurio ya
watazamaji uwanjani kutokana na wengi kutokwenda wanapojua itaonyeshwa
katika Televisheni. Sanga alimalizia kwa kusema ni afadhali kituo hicho
kingekuwa kinawapa fedha kufidia hasara hiyo. Wewe ni shabiki wa Yanga?
Nini maoni yako.
No comments:
Post a Comment