Wednesday, 10 April 2013

DO YOU KNOW THAT..........

TAARIFA KUTOKA NEWSROOM.
WABUNGE wamepitisha marekebisho ya kanuni za Bunge kifungu cha tisa kinachohusiana na masuala ya Fedha.
Akiwasilisha hoja hiyo katika mkutano wa 11 wa Bunge , Naibu Spika wa Bunge Job Ndugai ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati za Bunge amesema lengo la mabadiliko hayo ni kutoa nafasi kwa wabunge waweze kuishauri Serikali kuhusu mwenendo mzima wa Bajeti kabla ya bajeti yenyewe haijawasilishwa.
Aidha Mbunge wa Wawi Hamad Rashid Mohamed amempongeza Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano na Serikali kwa kufanya mabadiliko ya kanuni kuhusu utaratibu wa mapato na matumizi ya Bajeti.
Kutokana na mabadiliko hayo Bajeti za Wizara mbalimbali sasa zitasomwa mwezi April badala ya mwezi June na Wizara ya fedha ndio itakuwa ya mwisho kusomwa bajeti yake baada ya Bajeti za Wizara nyingine hivyo kutoa fursa kwa Bajeti kuanza kutumika mapema kuanzia terehe Mosi ya Mwezi July.
****
IMEELEZWA kuwa tatizo la wapiga debe katika vituo vya mabasi na daladala nchini linaweza kumalizika endapo Halmashauri za Miji na Majiji zitatimiza wajibu wake ipasavyo kwa kuwaondoa na kuwachukulia hatua za kisheria wapiga debe wanaofanya kazi katika vituo hivyo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na majini nchini Sumatra Ahmad Kilima akizungumza na kituo hiki amesema wao hawahusiki moja kwa moja na kuwaondoa wapiga debe vituoni kama ambavyo
watu wengi wamekuwa wakifirikiali
Amesema endapo mamlaka hizo zitashirikiana ipasavyo na wananchi likiwemo jeshi la polisi nchini, tatizo la wapiga debe litaisha na kuondoa kero kwa abiria na wasafiri wanaotumia vituo hivyo ikiwa pamoja na kupunguza wizi na udokozi unaofanyika katika vituo hivyo.
****
JESHI la Polisi nchini kwa kushirikiana na mikoa na halmashauri za Miji na Majiji limesema lina mpango wa kuanzisha utaratibu wa kuweka alama katika bodaboda ili kubainisha maeneo zinapofanyia kazi kwa
lengo la kupunguza uharifu.
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema ameieleza TIMES FM kuwa kupitia mpango huo utasaidia kubainisha bodaboda ambazo zimekuwa zikikiuka sheria na kutumika katika matukio ya uharifu ikiwemo ujambazi.
Amesema mpango huo pia utawezesha watumiaji na vikundi vya bodaboda kutoa taarifa za matukio ya uharifu unaofanywa na majambazi kwa kutumia boda boda ikiwa pamoja na kukomesha wizi wa pikipiki hizo.

No comments: