Saturday, 10 August 2013

HAYA SASA DIAMOND KAFANYA TENA MAMBO MOMBASA AWAACHA BADO NA KIU



Ni jambo jema kumshukuru Mungu kwa kumaliza mfungo
huu wa Ramadhani pia kutuweka salama hadi leo...
Sikukuu yangu nimeilia nchi Kenya lakini nilikuwa na
kibarua kukonga nyoyo za maelfu ya mashabiki zangu
jijini Nairobi.Kwangu hii ilikuwa mara ya pili kufanya show
 kenya,lakini ni mara ya kwanza kabisa
kufanya show jijini Nairobi,kutokana na kiu ya mashabiki
 zangu nchini humo nikaona zawadi ya Eid hii
iwadondoke wao.....It was crayzz yanii niliposhuudia umati wa
 watu wakiimba nyimbo sambamba na mimi,na kufurika hadi getini
kiukweli nilifurahi sana kwa hali iliyokuwa usiku wa jana.....
Nikiwa na team yangu nzima ya wasafi,stejini na
silaha zangu 4 hatari kwenye Mashine alikuwepo
Dj Rommy Jones kama kawaida stage manager
Qboy msafii alikuwepo kuhakikisha usalama upo saawia kabisa.....!!

UNAWEZA CHEKI PICHA KADHAA ZA TUKIO ZIMA
 LA SHOW NCHINI KENYA
KWENYE SIKUKUU YA EID...
..
Backstage nikisubiria go ahead nikafanye maujanja yangu kwa steji...
Ajajajaja....hapo sasa,ndo vile twafanyaga kwa jukwaaaa.....

Qboy Msafii & Dj Rommy Jones...

Ebhana eeeh watu bado wanataka niendeleee.....mpera mpera
 tu,afe kipa afe beki lakini ushindi lazima


Siwasiki watu wangu wa Nairobi.....nimekuja kuwabamba ile mbaya....
Tumeelewana watu wangu wa kweli........Mi naona kama muda umeisha vile....
Si ndo mashetani ya kigoma yakapanda ni kuanza kuwapelekea
kama Bongo tu...

Thursday, 8 August 2013

HILI NDO JAMBAZI SUGU LA ATM DAR ES SALAAM LILILO NUSURIKA KUUWAWA



Dar es Salaam. Msako wa wezi wa kwenye Mashine za Kutolea Fedha (ATM), umeanza kuzaa matunda baada ya raia wa Bulgaria kukamatwa akiiba kwenye ATM ya Bank of Africa (BOA), Tawi la Afrikana, Kinondoni, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa za benki, mtuhumiwa huyo ambaye 
hakutajwa jina lake alikamatwa baada ya kamera maalumu zilizowekwa kwenye ATM za BOA, kumtambua kuwa ni mwizi sugu wa benki hiyo anayetafutwa.
Mmoja wa wafanyakazi wa benki hiyo ambaye hakupenda kutajwa jina kwa kuwa si msemaji, alisema tukio hilo lilitokea jana saa 12 asubuhi baada ya mtuhumiwa huyo kuwekewa mitambo maalumu ya kumnasa.
Alisema benki hiyo ilipelekewa malalamiko na baadhi ya wateja kwamba wakienda kutoa fedha kwenye ATM wanakuta akaunti zao hazina salio wakati wanaamini zilikuwa na fedha.
Chanzo hicho cha habari kilidai kuwa baada ya kupelekewa malalamiko hayo, waliweka mitambo maalumu ya kuwawezesha walinzi wa maeneo ya ATM za BOA kumbaini mtu atakayetoa fedha kwa njia ya wizi.
“Kama Benki tuliweka mtambo maalumu na mtuhumiwa huyo alionekana kwenye mtambo wetu, hivyo tuliwaagiza walinzi wetu watakapomwona mtu huyo wamkamate haraka sana,”alisema.
Alisema mtuhumiwa huyo alianza mchezo huo kwa muda mrefu ambapo kwa kutumia kadi za ATM zisizojulikana idadi yake, alikuwa anakwenda kwenye ATM mbalimbali za benki hiyo na kutoa fedha hadi Sh10 milioni.
Kuhusu tukio la jana, mmoja wa walinzi wa BOA aliyejitambulisha kwa jina moja la Frenky alisema mtuhumiwa huyo alipofika kwenye ATM hiyo aliingia na kuchukua fedha ambazo alizipeleka kwenye gari lake. Frenky alisema baada ya kupeleka fedha hizo, alirudi kwa mara ya pili ili achukue fedha nyingine ndipo walinzi hao walimkamata na kumfunga pingu.
“Huyu mtuhumiwa mwenye asili ya Kiarabu alifika na gari lake saa 12 asubuhi, aliingia kwenye ATM na kutoa fedha ambazo hazikujulikana ni shilingi ngapi na kuzipeleka kwenye gari lake, baadaye alirejea tena kwa ajili ya kutoa fedha zingine, wakati anaingia ndipo alipokamatwa na mlinzi aliyekuwa analinda hapo,” alisema Frenky.
Kamanda wa Polisi Kinondoni, Camilius Wambura alikiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa anashikiliwa na jeshi hilo huku uchunguzi dhidi yake ukiendelea.
“Ni kweli taarifa nimezipata, mtuhumiwa amekamatwa, bado hatujajua ni kiasi gani ambacho ameiba kwa kutumia mtandao, tunaendelea na uchunguzi,” alisema Wambura.
Tukio kama hili lilishawahi kutokea mkoani Mwanza Februari 19 mwaka huu na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kushirikiana na maofisa ya Benki ya NMB liliwatia mbaroni watu watatu ambao walidaiwa kuiba kiasi cha Sh700 milioni kwa nyakati tofauti

Tuesday, 6 August 2013

DIAMOND NOMA SANA: ONA ALICHOKIFANYA SOUTH AFRICA ALAFU MSEME DIAMOND ANALOGA-HARD WORK PAYS BWANA


Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini kishule na kikazi pia. Staa huyo wa Kesho ameshoot video ya wimbo wake mpya ambao bado haujulikani ni upi mpaka sasa.
Hata hivyo tofauti na video zake za awali, hii mpya amekata kisu kirefu zaidi kwa kushoot na miongoni mwa gari yenye thamani zaidi duniani, Ferrari. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa gari hiyo inayotengenezwa na Waitaliano, imewekewa namba za gari binafsi kwa kuandikwa ‘Platnumz’ na Wasafi’.
0b54d01efdd411e2bd3c22000ae90db5_7
Mafundi wa Afrika Kusini wakihakikisha plate ya Wasafi imekaa vizuri
0f7a71cefdef11e2999e22000a1f8afc_7
dd5ff8c8fdce11e2aa0322000a1fa408_7
Inaonekana hii, Diamond Platnumz aka Coca Boy amejiandaa kwenda international zaidi.
Picha: Babutale (Instagram)
Source:Bongo5

PETER OKOYE WA P SQAURE AMPA DEMU WAKE RANGE ZAWADI YA KUMPENDA



With so Little to Say But Much To Express…….Peter ”P-Sqaure” Okoye Got Engaged to Lola OmoTayo his longTime GirlFriend and baby Mama….Peter proposed to the mother of his two children with a brand new Range RoverPictures : Peter P Square Okoye Engagement gift to Lola omotayo


                                    Pictures : Peter P Square Okoye Engagement gift to Lola omotayo


Pictures : Peter P Square Okoye Engagement gift to Lola omotayo

Saturday, 3 August 2013

ROSE NDAUKA AWASHUKIA WALIOZUSHA NA KUSEMA ALIINGIA GESTI NA MSANII WA BONGO FLAVA



Mwanadada Rose Ndauka amewawakia baadhi ya waandishi wanoandika habari zauongo kuhusu yeye kufuatia hivi karibuni kuripotiwa kuwa amekutwa kaitika nyumba ya wageni akivunja amri ya sita na mwanamziki mmoja wa muziki wa kizazi kipya.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao mmoja wa kijamii Rose aliandika

Dah magazeti yanapenda chokochoko kweli haswa wakimuona mtu katulia....kama hujui uliza sio tu unaongea au unaandika kitu ambacho ukijui......mnaudhi sana

Huku akionesha picha ya gazeti moja la udaku lilikouwa na habari hiyo.



Hapo awali iliripotiwa na baadhi ya mitandao ya habari na baadhi ya magazeti kuwa mwanadada huyu alionekana akipapaswa ndani ya gari na baadaye yeye na mwanamuziki huyo aliyotajwa kwa jina la dogo  Nasry kwenda kuvunja amri ya sita katika hoteli ya chumba hicho.

Source:Bongo Movies

ALIYEKUA MWANAFUNZI WA ST. JOHN UNIVERSITY ASHIDWA MSOSI NCHINI INDIA AMKUMBUKA BIBI ESTHER CHAMWINO

 
PAUL MASELE aliekua mwanafunzi wa st john university of Tanzania ambaye kwa sasa yupo inchini india akijiendeleza na masomo ameshindwa kula chakula cha india na kukiri kukumbuka cha kula cha mama maarufu mitaa ya chamwino dodoma BIBI ESTHER nakuamua kuingia jikoni mwenyewe nakuangusha ugali wa nguvu  angalia picha









SOUCRCE; ANYALOV

Friday, 2 August 2013

DIAMOND! MWAMBIE ZITTO KABWE AFANYE SIASA AACHANE NA BONGO FLAVA"NEY WA MITEGO



Mfalme wa kudiss Tanzania, Nay wa Mitego amerejea tena kuchafua hali ya hewa kwa kutengeneza mijadala kwenye radio na kwenye mtandao kwa ngoma yake mpya, Salam Zao.


Kwenye Salam Zao, Nay ameendeela kufanya kile akifanyacho kwa uzuri (do what he does best) kuponda.
 
Awamu hii list ya aliowadiss imeongezeka zaidi na kuingia pia kwenye siasa huku akiendelea kuwapa madongo wana hip hop wenzie.


Ameanza kwa kumdiss Madee kwa kusema kuwa yeye ndio rais wa Manzese na kwamba Madee amesanda. “Mi ndo rais wa Manzese yule tozi kasanda, Manzese mikono juu naiongoza kamanda,” anachana Nay.


Nay wa Mitego ameendelea kuwadiss wana hip hip huku akiijita kuwa yeye ndio gangster rapper na anatengeneza hela huku wengine wakinuka vikwapa. Hakusita pia kuwarushia bombshell Weusi. “Yo Mchomvu wape salam ‘Kubumkubum’ waimbie watakufa njaa muziki umebadilika,” anarap Nay.



Nay pia amemdiss Zitto Kabwe kwa kurap:
 
 “Word up Diamond, mwanangu wewe si mtoto wa Kigoma, mpe salama Zitto Kabwe mwambie afanye siasa aachane na Bongo Flava huku hatumtaki kabisa, maneno mengi, propaganda hajui kutekeleza, Kigoma Allstars tayari kawatelekeza.”

Rapper huyo pia amerap kuwa wapo watu waliojipatia utajiri kutokana na misiba ya Mangwea na Kanumba.


“Wanamiliki gari, wameota na vitambi kwa hela za rambirambi, mkizingua nawataja,”anasisitiza. Anasema tangu kifo cha Kanumba Bongo Movies imekufa na haiuzi tena.


Pia hajamuacha mwanzilishi wa shindano la Bongo Star Search Rita Paulsen kwa kudai kuwa licha ya kuwapa zawadi kubwa washindi, wameendelea kupigika mtaani.

“Hizi Salam ziende kwa madam Rita na Bongo Star Search. Mshindi analipwa nini mbona kama magumashi?! Namuona Walter Chilambo kapigika kama zamani, Haji Ramadhani kachoka yupo kitaani. Nauliza milioni hamsini zao anazila nani, acheni ubabaishaji wekeni mambo hadharani.”



Source:Mpekuzi

SINTAH "SISI MASTAA WENYE MASTERS DEGREE HATUWEZI PIGIZANA KELELE NA MASHOROKO MEGENI"



Sintah leo kaja na haya : jisomee mwenyewe

"Ukifungua gazeti la babkubwa toleo jipya ,kurasa ya katikati shurti utakutana na kichwa cha habari MASTAA Ambao shule imelala kichwani, seriously kuna siku mdau alinitumia comment maana mimi na magazeti ni hasi na chanya, 
kilichoandikwa ni ukweli mutupu jamani khaaa sasa mtu mwenye MA apigizane kelele na mashoroko mageni aaaah wapiii??

though babkubwa mmejichanganya sana maana mmeandika ndivyo sivyo one n only CEO anayetambulika ana MA International Relations and Diplomacy naomba ieleweke hivyo, sijui kwa wengine mliowaja kama ni sawa ama ila me mmenimixia sana na ma post graduate ya nini mieee?

 CEO's 
MA International Relations n Diplomacy
BA Public Administration and Management  (kwa wale ambao mme cram  BA hamkawii kusema Business Admin khaaaa ni Bachelor of Arts in PAM muelewe sasa.

hope tumeelewana ila sivibaya nikawataja na wenzangu ambao tuna hadhi ya kipekee (sio mchezo,, sonyaa, kwanini ilikushinda kama ni rahisi?? ukipata jibu utakuwa umenielewa chezeyaa kufanya research weweee)

Mwegelo Jokate 
Black Rhino
Dj Fetty
Nikki wa Pili
Hamisi Mwinjuma
Ally Remtullah
na mwenyewe CEO wa ukweeeh 

UJUMBE
unaweza ukawa kama  hao hapo juu ila acha majungu, umbea, fitina, hela unazozipata kama ni mwanadada usijipeleke kununua lace wig, sijui Galaxy zichange mdogo mdogo ujitupe kile chuo kinaitwa V*** fasta .

The roots of education are bitter, but the fruit is sweet.

okaybyeeee..
Swaum Maqbul" Sintah

BAADA YA ROSE NDAUKA KUHUSISHWA KATIKA FUMANIZI...!! HAYA NDIYO MANENO YA MCHUMBA WAKE ROSE KUHUSU SAKATA HILO



BAADA ya msanii wa filamu nchini Rose Ndauka kuripotiwa kufumaniwa akiingia gesti na msanii chipukizi wa muziki wa bongo fleva Nassoro Ayoub 'Dogo Nasry' huku akiwa amevaa baibui kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani,  mumewake mtaarajiwa Maliki Bandawe 'Chiwaman' amjia juu msanii huyo kwa madai ya kumchafua mpenzi wake.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Chiwaman aliweka wazi kuwa msanii huyo Nasry ambaye alimuomba Rose aweze kushiriki kwenye video yake, walishindwa kufikia maamuzi kutokana na kiwango cha malipo kuwa madogo, na badala yake msanii huyo alimuomba wapige picha kama ukumbusho.

Alisema kuwa kitendo hicho cha kupiga picha na msanii huyo wakati wapo katika mazungumzo ya awali ya kukubaliana malipo ndizo picha alizotumia msanii huyo na kudai kuwa alikuwa naye nyumba ya wageni kitendo ambacho si cha kweli.

"Hawa wasanii wachanga wanatafuta umaarufu vibaya kwa kuwachafua watu, ilikuwa amemuomba Rose ashiriki kwenye video yake na ndipo walipokutana kwa ajili ya mazungumzo hayo na alikuwa na mdogo wangu sasa hapo masuala ya gesti yametokea wapi" alisema Maliki.

Aliongezea kuwa "kama nilikuwa sijui hicho kitu na kwa jinsi mambo yalivyokuwa ningeweza kumuacha mchumba wangu ninayempenda kwa dhati, ila msanii huyo alichokifanya siyo jambo sahihi, kwani alimuomba apige naye picha na Rose alikubali huku bila kujua nia yake ".

Maliki alisema kuwa huyo msanii anatafuta umaarufu kwa kuchafua majina ya watu wengine, kitu ambacho hakina mashiko kwenye jamii.

ROSE NDAUKA ANASWA AKIPAPASWA NDANI YA GARI KABLA YA KUPELEKWA HOTELINI



Rose Ndauka  au  Aisha  anaweza  kuwa  ameitia  najisi  funga  yake  baada  ya  kunaswa akiingia  hotel  moja   iliyoko  kinondoni  jijini  Dar  kwa  kile  kilichoelezwa  ni  kwenda  kuivunja  amri  ya  sita  na  mwanamziki wa  bongo  fleva  Nassoro  Ayoub  "Nasry"   au  Tajiri Boy
Rose ambaye alisilimu mwaka jana  na  kupewa  jina  la  Aisha  baada  ya  kuchumbiwa  na mwanamziki  mwasisi  wa  kundi  wa  TNG Squad, Malik Bandawe, alifumwa na  kamera  za wakazi wa jirani na  hoteli  hiyo  mwishoni  mwa  wiki  iliyopita.....



Shuhuda  wa  tukio  hilo  amedai  kwamba  majira  ya  mchana  kweupe  gari  aina  ya  Toyota Mark  X lenye  rangi  nyeusi  liliwasili  kwenye  viunga  vya  hoteli  hiyo  na  kusimama  kwa  takribani  dakika  10  kisha  likaondoka  na  kwenda  kupaki  sehemu  nyingine  ambapo  ni  umbali  mfupi  toka  hotelini  hapo...

Kitendo  hicho  kiliibua  mashaka  miongoni  mwa  watu  hasa  kutokana  na  vioo  vya  gari  hilo  kuwa  tinted  hivyo  kutowaonesha  waliokuwemo  ndani...

"Walipoondoka  na  kupaki  palipojificha  tuliamua  kuwasogelea  ili  tujue  ni  akina  nani

"Baada  ya  muda, kioo  cha  dereva  kilishushwa kidogo, tukamuona  dogo  anayefanana  na Diamond  akiwa  anampapasa  demu  aliyekuwa  pembeni  yake...

"Tulipoona  hivyo, tulidhana  mnyamwezi  ameamua  kumaliza  mambo  yake  ndani  ya  gari, hivyo  tukaziweka  simu  zetu  standby  kwa  ajili  ya  kushuhudia" alisema shuhuda  huyo

Baada  ya  muda, mlango  wa  kulia  ulifunguliwa  kisha  wakamuona  dogo  aliyetambuliwa  kwa  jina  la  Nasry

"Kumbe  hakuwa  Diamond,alikuwa  ni  dogo  Nasry.Tulipotupa  jicho  ndani, tulihamaki  kumuona  Rose  Ndauka  akibadili  nguo  na  kujitanda  baibui. 

"Nadhani  alifanya  hivyo  ili  watu  wasimjue  pindi  atakaposhuka  kwenye  gari  maana  aliposhuka  tu, waliongozana  na  dogo  Nasry  kwa  mwendo  wa  kasi  hadi  ndani...


"Toka  walipoingia  ndani  hadi  walipotoka  iliwachukua  kama  masaa  matatu  hivi.Wakati  wa  kutoka, Nasry  alilifuata  gari  hadi  mlangoni  na  kisha  Rose  akaingia  na  kutokomea"...Kilimalizia  kusimulia  chanzo  hicho

Source: KIU

HABARI KUHUSU ALLY KIBA KUKAMATWA NA DAWA ZA KULEVYA AMSTERDAM Ally Kiba


Ally Kiba Siku hizi Tanzania kumekua na mambo meeeengi yanayozushwa au kuanzia kwenye mitandao ya kijamii sanasana facebook na twitter ambapo miongoni mwa makubwa ya wiki hii ni stori kwamba mwimbaji wa Bongofleva Ally Kiba amekamatwa na polisi wa Amsterdam kwa tuhuma mbalimbali na wengine walidiriki kuripoti kwamba ni dawa za kulevya.
Ally Kiba mwenyewe aliandika kwenye page yake ya twitter kama kukanusha lakini ni tweet ambayo haikuwa rahisi kuielewa au kufahamu alichomaanisha kama unavyoona hapa chini..
Ally Kiba akanusha kukamatwa na polisi Amsterdam July 25 2013 1 
Baada ya hii tweet ilibidi millardayo.com imuendee inbox au DM kumuuliza kama ni kweli alikamatwa ambapo hili ndio jibu lake….
Ally Kiba akanusha kukamatwa na polisi Amsterdam July 25 2013 2

Huenda siku kadhaa zijazo Tanzania ikapata sheria mpya itakayokua inadili na watu wanaoitumia vibaya mitandao kama vile kutukana, kuandika uongo na mengine kama hayo… July 26 2013 Wakili Mwandamizi wa Serikali alisema makosa ya kwenye Internet yameongezeka sana Tanzania na hakuna sheria inayodili nayo moja kwa moja hivyo kuna mpango wa kuipata sheria ya hayo makosa .

Source:Millard Ayo

WEMA SEPETU KUIVAMIA BONGO FLAVA "SNURA NA SHILOLE TUPA KULE"



Wema Sepetu miss Tanzania aliyegeuka kuwa muigizaji, ameweka wazi kwamba anataka kuimba na katika kuthibitisha hilo ameshaandika mistari kadhaa ya anachotaka kuimba. Wema alishawahi kuimba kwenye wimbo wa kuhamasisha kumchangia msanii Sajuki wakati anaumwa. Wimbo huo unaitwa “Mboni yangu”, so kuingia kwenye booth kurekodi wimbo sio kitu kipya kwa Wema Sepetu. Hii ni baadhi ya mistari ambayo ameshaandika Wema Sepetu kwa ajili ya wimbo huo.
Mwambie wake ni mimi, na kwangu moyoni atabaki ni yeye, tena mwambie bado silali kutwa nawaza penzi langu… ila siku atakugundua kuwa mi ndo mwenyewe
Mpaka sasa hivi ni wimbo mmoja Wema alirekodi kwa kushirikiana na Snura ambapo Tunda Man alishiriki pia kuuandika

MZIMU WA KIFO BADO WAZIDI KUWATAFUNA WASANII WA BONGO,SASA MAMA WA SUPER STAR WA SHAA..!!



Mwanamziki SHAA ambaye anafanya Game ya Muziki wa Bongo Fleva, Amefiwa na mama mzazi.
GUMZO LA JIJI linatoa pole sana kwa Shaa pamoja na Familia yake. Mungu ampe Nguvu katika kipindi hiki cha Msiba.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.
R.I.P Mama Shaa.

Monday, 29 July 2013

AZZAN:NITAJIUZULU IKIBAINIKA NIUZA MADAWA YA KULEVYA



MBUNGE wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, amesema yupo tayari kujiuzulu ubunge, ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan. Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu sakata hilo, alisema hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla.

Alisema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake, ni wazi amedhamiria kumshushia heshima na huenda akawa ana jambo limejificha.

“Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwanini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo.

“Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.

“Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernad na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.

“Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu,” alisema Azzan.

Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.

“Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni,” alisema Azzan.

MTANZANIA ilipomuuliza kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, alisema atakachokifanya anamuachia Mungu.

“Ni ngumu kusema hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua,” alisema Azzan.

Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa kupitia mitandao, ziliripoti kukamatwa kwa Watanzania wawili nchini China wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Dola milioni 3.34 za Marekani.

MASOGANGE BALAA JIPYA,MAHAKAMA YAMFUTIA DHAMANA ARUDISHWA LUPANGO


HUKU  akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepata balaa jipya,GUMZO LA JIJI lina taarifa kamili... 
   

 

                          Dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo, Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
KWA NINI DHAMANA IFUTWE?
Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.
“Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.

“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.
“Hii inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa, ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.

MASOGANGE AKAUKA MITANDAONI
Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
“Nyiye si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.

WABONGO WALIOJITOLEA FEDHA KUMWOKOA WASIKITIKA
Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.
Kamanda Nzowa.
SHERIA ZA AFRIKA KUSINI NA TANZANIA KUHUSU ‘UNGA’ SI SAWA?
Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande.

POLISI HAWAKAUKI NYUMBANI KWAKE
Habari kutoka vyanzo vya hapa Bongo zinadai kuwa, askari polisi (kituo cha kazi hakijajulikana) wamekuwa wakifika nyumbani kwa msanii huyo, Kijitonyama, Dar na kuwauliza mambo kadhaa majirani.
“Jamani ishu ya Masogange vipi? Maana hapa mtaani kuna polisi wamekuwa wakija mara kwa mara na kumuulizia kama yupo. Wao hawajitambulishi kama askari lakini watatu kati yao wamebainika ni polisi,” kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea kudai kuwa, Julai 20, mwaka huu alifika askari mmoja na kuuliza majirani kama wamewahi kumwona mwanaume mrefu, mweupe akiingia kwenye nyumba ya Masogange.
“Julai 20 alikuja afande mmoja, akawauliza majirani kama kuna siku yoyote ambayo mwanaume mrefu, mweupe aliingia kwa Masogange, akajibiwa hajawahi kufika mtu wa aina hiyo.
“Ndiyo maana nikauliza kesi yake vipi kule Bondeni (Afrika Kusini)? Ila kuna kitu nilikisikia kwa baadhi ya watu kwamba kuna ndugu yake atakuja kuhamisha vyombo vyake kwa sababu wanajua kesi itachukua muda mrefu,” kilisema chanzo.
Masogange.
KUMBUKUMBU
Julai 5, mwaka huu, Masogange na Melisa walinaswa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo mjini Kempton Park, Afrika Kusini.
Ilidaiwa kuwa thamani ya mzigo huo wenye kilo mia moja na hamsini ni shilingi bilioni moja na laki sita..

DIAMOND PLATNUMZ AENDA SHULE SOUTH AFRICA KUONGEZA VIDATO


The Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini alikoenda kuongeza vidato kidogo. Apparently, hitmaker huyo wa Kesho amejiunga na chuo ambacho hakijajulikana jina lake bado na hajasema ameenda kusoma nini.

Kupitia Facebook, staa huyo amewauliza mashabiki wake wabashiri ameenda kusoma nini chuoni hapo na haya ni baadhi ya majibu.

Faiso Yahya: Ka si english course basi unenguaji

Galus de Focus: HOTEL MENEGEMENT

Benjamin Osarya Jr.: Unasoma matangazo….kwenye notes board.

Nelson Choka: Samahan form 4 umemaliza ww et..!! Labda una risit dogo mh

Rose Selestini: Unatafuta wadada wa chuoni.

Christian Biseko: wa kusoma uwe wewe??? Elimu siyo mchezo wewe!!!

Gara B Kubwa: English Course ili Ushiriki BBA mwakani…una Mbwembwe dogo wewee..

Emmanuel Makaga: Unasomea jnc ya kubun skendo mpya kwny mass media

Gabrie Lbrighton: Wanaosoma hawajitangazi wew may be ungetuambia akitoka huyu mwanamke uliye nae nani anafata.
Nàdhifá Dórnald Unasomea mapenz maana unayapenda sana

Sunday, 28 July 2013

SOMA BARUA ILIYOANDIKWA NA MFUNGWA WA MADAWA YA KULEVYA KUTOKA TANZANIA HUKO HONG KONG-MBUNGE KATAJWA

Below is one drug mule story, the story of mules from Tanzania entering Hong Kong. Because of its location on the East coast of Africa, Tanzania is the favorite launching place for drug lords to mission their mules. The drugs they carry are mainly from Pakistan and Afghanistan....taken by boat to Tanzania ....meeting small boats along Tanzania's long coastline

In Hong Kong there are currently about 200 inmates from Tanzania. About 130 convicted and about 70 on remand  (...unofficial figures..). In May-June 2013, some 50 Tanzanians were arrested in Hong Kong and China

Those convicted serve a minimum time of about 9 years if they plead guilty. They serve 21 years if they don't plead guilty (but drugs are found in their possession)

The story of these Tanzanian mules entering Hong Kong is typical of what happens around the world. Hopefully this story will be seen by many people in Africa, especially in Tanzania, and will discourage others from becoming mules. If this article stops even one person from being a mule, it is worthwhile
 Here is the story, written in Swahili by a Hong Kong Tanzanian inmate, translated into English by another inmate. The story names and shames some very important people in Tanzania:





Wednesday, 24 July 2013

JEURI YA FEDHA WEMA SEPETU AVUTA MKOKO UNAOENDANA NA RANGI AIPENDAYO ZAIDI KATIKA MAISHA YAKE


Haya ndio Maneno ya Martin Kadinda aliyoandika facebook na kuweka picha ya Wema akiwa na gari hilo

"samahani kwa ubora wa picha kuwa hafifu....... Ila huyu dada anapenda pink kupitiliza..... haya she gat new pink Car.... mkutane barabarani..." aliandika Martin