Tuesday, 4 June 2013

P FUNK APAGAWA BAADA YA KUONA JENEZA NGWEAR

P Funk Majani akisisitiza jambo                 Editruda Mashimi,Dar es Salaam
MWANDAAJI wa ala za muziki nchini Tanzania  P Funk Majani alichanganyikiwa baada ya kuona jeneza iliyokuwa imebeba mwili wa aliyekuwa msanii wa muziki wa kizazi kipya Albert Mangwea.
P Funk ambaye muda wote alikuwa amekaa kwenye gari akiwa na huzuni mkubwa kufuatia kifo cha msanii huyo, alibadilika ghafla baada ya kuona jeneza hilo likiingizwa katika gari maalum tayari kwa ajili ya safari kwenda katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
P Funk alishindwa kujizuia na akalazimika kushuka kwenye gari lake na kwenda kusukuma gari lililokuwa limebeba mwili wa msanii huyo aliyefariki Dunia Mei 28 mwaka nchini Afrika Kusini.
Kitendo cha P Funk kusuka gari hilo huku akibubujika machozi kwa zidi ya dakika mbili ilihamasisha mashabiki wa msanii huyo na kuungana naye kusukuma gari hilo.
Tukio hilo lilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, wakazi wa jiji la Dar es Salaam kesho watapata fulsa ya kutoa heshma ya mwisho kwenye jeneza la marehemu Mangwea katika Viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam kabla ya kusafirishwa kwenda Mjini Morogoro kwa mazishi kesho kutwa.

PHOTO: MWANADADA MTANZANIA ATAKAYENYONGWA MISRI IJUMAA HII


You might also like:

Monday, 3 June 2013

AMMY NANDO WA TANZANIA NDANI YA BAFU MOJA NA MREMBO WA NAMIMBIA....



Jana (May 29) ilikuwa ni usiku wa tatu katika jumba la big brother Afrika huko Afrika Kusini mengi yanazidi kuonekana na sasa washiriki wengi wanaanza kuonesha side B ya mioyo yao na kujaribu kupata muda wa kuwa romantic na kuonesha upendo (Romantic time).

 Wakati washiriki wengine wakiendelea na mambo yao mtanzania Ammy Nando alijiachia kwenye bafu moja na na kuoga na mrembo Dillish kutoka na Namibia ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu akisomea Saikolojia.

Huenda huu ukawa mwanzo wa mahusiano yao humo ndani kwa sababu moyo hauna pazia na uzuri wa Dillish unaweza kumvuta to the limit model huyo wa kitanzania.

 Kwa upande mwingine the boss lady toka Kenya Huddah Monroe alipata nafasi ya kushare na  Denzel mawili matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel akiwa ameonesha tangu mwanzo kudata kwa Huddah. 



Jana Huddah alifunguka na kumwambia kuwa anahitaji mwanamme mwenye pesa na kwamba she is a gold digger.
 

Wiki hii Benzel, Betty, Huddah, Selly na Natasha wako katika nafasi ya  kukumbwa na Eviction

VIDEO  YAO:

BIG BROTHER: MSHIRIKI WA TANZANIA APEWA KAZI YA KUTEMBELEA MIGUU NA MIKONO KWA MUDA WA SIKU TANO


SHINDANO la Big Brother Afrika limeendelea kwa washiriki wawili kutolewa katika wiki ya kwanza ya mchezo huo ambao unashirikisha washiriki wapatao 28 kutoka nchi 14 barani Afrika.

 Jumatatu iliyopita washiriki walipata nafasi ya kutoa mapendekezo yao ya kuchagua washiriki ambao wanaona wanafaa kuingia katika Danger Zone ambapo watano kati yao ndio waliotajwa mara nyingi zaidi na washiriki wenzao hivyo kuingia huko. 

Washiriki waliongia katika Danger Zone walikuwa ni Betty wa Ethiopia, Selly wa Ghana, Denzel wa Uganda, Natasha wa Malawi na Huddah wa Kenya ambapowatazamaji walitakiwa kumpigia kura mshiriki ambaye wanaona anafaa kubakia ndani ya jumba hilo. 

Katika kura zilizopigwa na watazamani kutoka nchi 14, Betty ndio alipata kura nyingi zaidi baada ya kupata kura 5, akifuatiwa na Selly na Natasha waliopata kura tatu kila mmoja huku Denzel na Huddah wao wakiambulia kura mbili hivyo kumaanisha kwamba safari yao katika kugombea dola 300,000 kuishia hapo.
 
 Baada ya kutolewa katika jumba hilo IK mtangazaji wa kipindi hicho aliwapa nafasi washiriki hao kulipa kisasi kwa kuchagua mshiriki mmoja ambaye hupewa kazi ambayo hutakiwa kuifanya kwa muda atakaopangiwa.
 
Wa kwanza alikuwa Denzel ambaye alitakiwa kuchagua mshiriki ambaye atatakiwa kila akitoka nje kupunga hewa kwenye jumba hilo awe anatembea kwa miguu na mikono kwa muda wa siku tano na kijana huyo hakusita kumchagua Nando mshiriki wa Tanzania kufanya kazi hiyo. 
 
Aliyefuata alikuwa na Huddah ambaye yeye aliambia achague mshiriki ambaye atakuwa akitandika vitanda vyote katika jumba hilo kwa muda wa siku mbili na mwanadada huyo mrembo kutoka Kenya alimtaja mwanadada mwenzake Dillish kutoka Namibia kufanya zoezi hilo. 
 
Shindani hilo linaendela tena leo ambapo washiriki watatakiwa tena kupendekeza majina ya washiriki ambao wataingia katika Danger Zone kwa ajili ya kupigiwa na mashabiki ambapo atakayepata kura chache ataliacha Jumba hilo Jumapili ijayo.
pro24

VIDEO: HUU NDO UCHAFU UNAOTENDEKA NDANI YA JUMBA LA BIG BROTHER AFRICA

Hii ni video inayoonesha  uchafu  unaotendeka  ndani ya jumba la Big Brother Africa....
 
Nashindwa  kuusimulia, ila jionee mwenywe  katika  video  hiyo.....

COCACOLA WAMNUNULIA GARI JIPYA DIAMOND

Ukikutana na Diamond mtaani akiwa na mchuma mpya wenye rangi nyeusi, usishtuke sana, jua ni courtesy of Cocacola.
16859d0ccbab11e29f3f22000a1f978e_7
Inavyoonekana ni kuwa Cocaboy kama anavyojiita siku hizi, amenunuliwa gari jipya na wadhamini wake kampuni ya vichwaji ya Cocacola.
“Ya all ready know what it’s….. tukutane Fuel station!! #CocaCola Mumetishaaaaaa,” aliandika jana kwenye picha ya Instagram ya gari hilo likiwa na maganda yake.
 
“Chatin infront of my Small baby… on @channeloafrica interview at my clib,” aliongeza.

Siku nzima ya jana, hitmaker huyo wa Kesho alikuwa busy kwenye interview na kituo cha runinga cha Channel O.
af471706cb8211e2896422000a1fb003_7

ALBERT MANGWEA AAGWA NA WATANZANIA WALIOKO AFRIKA KUSINI.....MWILI WAKE UTALETWA KESHO SAA NANE


Watanzania waishio nchini South Africa wamepata nafasi ya kuuaga mwili wa Albert Ngwea kuelekea katika safari ya mwisho wakiongozwa na Msanii Bushoke na Mtoto wa Mhe. Kingunge Ngombale mwiru, Kinjeketile wanaosimamia mipango ya kuaga mwili nchini Afrika kusini...

Mwili  wa  marehemu  utaletwa Tanzania  kesho  saa  nane.....

WABUNGE WANASWA KATIKA DANGURO LA UCHI MJINI DODOMA....WALIKUWA WAKITOA PESA KWA KUZIWEKA MAKALIONI

Katika ukumbi maarufu wa muziki au kwa jina jingine ‘club’ (jina linahifadhiwa) uliopo mjini  Dodoma mengi yanatokea.

Watu wanaingia mmoja mmoja, wengine kwa makundi na baadhi wapo nje wakipunga kwanza upepo kabla ya kuingia.

Siku hizi wanawake wanaingia bure au kwa jina jingine ‘ladies free’ jambo linalosababisha ukumbi huu ufurike watu.

Katika ukumbi huu, yapo maeneo mawili. Kuna sehemu ya kawaida ambayo kiingilio chake ni kuanzia Sh5,000 hadi Sh10,000 kutegemeana na matukio au burudani ya siku hiyo.

Pia kuna eneo jingine ambalo ni kwa watu maalumu ama waweza kusema ni ‘VIP’ ambapo wateja wake hutakiwa kulipa Sh20,000.

Ukumbi wa VIP upo juu na ule wa kawaida upo chini. Hata hivyo maeneo yote haya hujaza watu kwa kiasi kikubwa.

Mwandishi wetu alifika katika ukumbi wa VIP saa tano usiku, hata hivyo bado watu ni wachache katika eneo hili ukilinganisha na kule kwa watu wa kawaida.


Ukumbi wa VIP si mkubwa kieneo . Kuna kaunta ya vinywaji, makochi madogo madogo aina ya sofa yenye meza mbele yake, viti vilivyoizunguka kaunta na katikati ya ukumbi huu kuna meza mbili za duara zenye mti wa chuma katikati.

Kadri dakika zinavyojongea, ndivyo watu wanavyoendelea kumiminika mmoja baada ya mwingine.

Saa saba za usiku ndipo Mwandishi wetu  aliposhuhudia kiongozi mmoja wa kitaifa ambaye hekima zake zinategemewa na Serikali na hata chama chake akiingia katika ukumbi huu akiwa na mabinti wadogo watatu.

Alipata nafasi ya kuketi, katika moja ya sofa zilizokuwa katika ukumbi huo, akaagiza vinywaji na kuendelea kunywa.

Muda wa saa saba, alitokea msichana aliyevaa sidiria na kisketi cha kujimwaga kifupi sana ambacho hata hivyo kiliuonyesha mwili wake waziwazi.

Msichana yule alipanda katika moja ya meza za duara zenye chuma na kuanza kucheza muziki uliosikika katika spika za ukumbi huo.

Baada ya kucheza kwa zaidi ya nusu saa, alivua kisketi cha rangi nyeusi alichokivaa na kukirusha… akabaki na nguo ya ndani aina ya ‘bikini’ ya rangi nyeupe, kisha akaendelea kucheza kwa kupandia vyuma katika meza hizo za duara. 

Baadaye alivua sidiria, akaendelea kucheza na kadri watu walivyokuwa wakimtunza fedha aliendelea kuonyesha ujuzi wake katika kucheza.

Baada ya muziki huo kukolea, msichana huyo alibadilisha mchezo, akalala kifudifudi na kuishusha nguo yake ya ndani hadi nusu ya makalio yake.

Wanasiasa waliokuwepo katika ukumbi huo pamoja na watu wengine walionekana kumpa fedha kwa kumwekea katikati ya makalio msichana huyo kadri walivyofurahishwa na uchezaji wake.

Wakati huohuo mwanasiasa mwingine kijana aliingia ukumbini hapo akiwa na rafiki zake na kuendelea kushuhudia dansi hiyo.

Baada ya kucheza kwa saa kadhaa, msichana yule alishuka katika meza, kisha akapanda msichana mwingine na kuendelea kucheza.

Aliposhuka, aliingia katika choo cha wanawake na kurudi akiwa amevaa suruali aina ya jeans na tisheti. Wanaume waliokuwa eneo hilo walimwita na kumpongeza, huku wakimnong’oneza maneno ambayo…yalikuwa siri yao.

Chanzo chetu cha habari kinaeleza kuwa wasichana hao ni raia wa Kenya ambao wanadaiwa kuwapo nchini kwa ajili ya kucheza dansi za aina hiyo.

“Wanafanya kazi ya kuhudumia wateja hapo kaunta, lakini unapofika wakati wa kucheza wanacheza,” kinasema chanzo hicho.

Kinaeleza kuwa pamoja na kulipwa kiasi cha fedha kama mshahara na wamiliki wa ukumbi huo, wasichana hao wanajipatia fedha wanazotunzwa wakati wa kucheza.

Chanzo kingine cha habari kinaeleza kuwa wasichana hao ni muunganiko au jumuiya ya vijana waliotoka nchi jirani kuja kufanya biashara hiyo ambayo imeshamiri nchini mwao.

Chanzo hicho kinaeleza kuwa, si wanasiasa hao waliokuwapo siku hiyo pekee, bali wanasiasa wa kiume kadhaa wenye majina nchini hufika hapo kutazama wanawake wachezao utupu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Hassan Ngwilizi, Mbunge wa Mlalo (CCM) anasema kwa kuwa wamefanya jambo hilo nje ya Ukumbi wa Bunge hivyo, hawastahili kuhukumiwa bali sheria inatakiwa kuwabana kama wananchi wa kawaida.

Hata hivyo, anasema kitendo hicho ni kinyume cha maadili na hakitakiwi kufanywa na viongozi kama hao.

Waziri wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe anasema sheria za nchi haziruhusu kumbi za starehe kuajiri watu wanaocheza utupu. Waziri Chikawe ambaye pia ni Mbunge wa Nachingwea anasema ni aibu kwa viongozi kutazama dansi za namna hiyo na baya zaidi kuwatuza fedha wachezaji.

“Wanapowatunza fedha, ni kama wanasifia hicho kitendo, ni kama wanasema hivi ndivyo inavyotakiwa” anasema Chikawe na kuongeza:

“Hata hivyo, wanapata wapi leseni za kuendesha huduma kama hizo?”

Anasema Tanzania ni nchi inayozingatia maadili ndiyo maana siku za karibuni Bunge lilipiga marufuku ‘kanga moko’ licha ya hao wacheza utupu.

Anaongeza: “Viongozi wanaotakiwa kuwa mfano wa kuigwa wanapoangalia dansi hizo, wanaendelea kumong’onyoa maadili”

Waziri Chikawe aliahidi kuzungumza na naibu wake, Angela Kairuki ili kuchukua hatua stahiki kwa klabu zinazoruhusu wasichana kucheza uchi.


Saturday, 1 June 2013

MSHINDI WA MISS VAA CONNECTION 2013 JOAN JOHN KUTOKA ST JOHN UNIVERSITY OF TANZANIA

Mshindi huyo wa miss vaa connection Joan John kutoka chuo cha st. John amejinyakulia kiasi cha fedha tshs milioni moja taslimu 1,000,000 na kua balozi wa VAA CONNECTION.

PICHA ZA KIJANA ADAM AKIONYESHA MANJONJO YAKE KATIKA EVENT YA VAA CONNECT DODOMA


MAMODELS WA VAA CONECT WAKITOA BURUDANI ANGALIA PICHA


MAJUDGE WA KITENGO CHA MAMODELS KATIKA PICHA



WANAWAKE WANAOJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA WAANDAMANA KUDAI HAKI ZAO HUKO AFRIKA KUSINI


Mengi kama haya tumekuwa tukiyasikia tukiyasikia yakitokea katika nchi zilizo bara la America na Ulaya, lakini sasa yameanza kutokea kwa nguvu zaidi katika bara letu lenye utamaduni wa kipekee na safi (Afrika) watu wanaojihusisha na mahusiano ya mapenzi ya jinsia moja wameanza kupaza sauti hadharani kuomba vitendo vyao vipewe baraka na vyombo vya dola.
Huko nchini Afrika kusini wanawake wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja (Lesbians) wamejitokeza hadharani kupinga sera za serikali ambazo hazizitambui haki zao wanazodai kuwa ni za msingi. Moja kati ya madai yao ni kutaka haki ya ndoa ya jinsia moja kuhalalishwa na pia waweze kurusiwa kuwa na wapenzi wao wa jinsia moja hadharani kama ilivyo kwa mapenzi tuliyozoea Africa kati ya watu wa jinsia tofauti.
 
Sera mapenzi ya jinsia moja lilianza kuwekwa hadharani na nchi za Ulaya kama Uingereza kwa kutaka  kushinikiza nchi za Afrika kubariki swala la ushoga la sivyo Uingereza itasitisha misaada kwa nchi zitakazopinga.
Eeeh Mungu tuepushe na hii hali, njaa ya misaada isitupeleke shimoni.

MABADILIKO: MWILI WA NGWEA UTALETWA JUMANNE NA SIYO KESHO


 Mwili wa ngwea  utaletwa Tanzania siku ya jumanne  na  siyo  kesho ...

Taarifa hizi nikwa mujibu wa tweet alotweet Millard Ayo aliyeko nchini africa kusini ulipo mwili wa marehemu Ngwair

MISS REDDS DODOMA 2013 HAPPINESS BAADA YA KUVISHWA TAJI

 


PICHA ZA WASHIRIKI WA MISS REDDS DODOMA SIKU YA TUKIO





HUU NDIO UKUMBI WA KISASA UNAFANYIKIA EVENT YA VAA ( vijana against aids) KATIKA CHUO CHA MIPANGO DODOMA


Siri kubwa ripoti, uchunguzi kifo cha Mangwea




Marehemu Mangwea (kulia) enzi za uhai wake akiwa na msanii M 2 The P,ambea pia alizimia akiwa na marehemu na kupata nafuu                   Pretoria,Afrika Kusini
WATANZANIA wanaoishi nchini Afrika Kusini na nchi jirani ya Botswana leo wamejitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea,kesho mwili wa marehemu unatarajia kuwasili nchini Tanzania na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa, kabla ya shuguli za kuuaga tena kufanyika katika Viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mangwea aliagwa na umati wa watu mbalimbali wakiwemo Watanzania na watu wa mataifa mbalimbali wanaoishi nchini Afrika Kusini, jijini Dar es Salaam pia kutakuwa na zoezi kama hilo siku ya Jumatatu kabla ya kusafirishwa hadi mjini Morogoro kwa mazishi siku ya Jumanne.
Pamoja na kwamba Mangwea anatarajia kuzikwa mjini Morogoro, utata juu ya ripoti ya uchunguzi wa kifo chake imeanza kutawala, baada ya kuwepo kwa mvutano wa kuifanya ripoti hiyo kuwa siri, huku baadhi ya watu wakitaka ripoti itangazwe kama ilivyoandikwa na jopo la Madaktari wa Hospitali ya  St Hellena Joseph.
Inaelezwa kwamba familia ya msanii huyo imekataa kuweka wazi sababu za kifo cha mtoto wao, "Ripoti ya Uchunguzi wa Madaktari imetoka lakini haturuhusiwi kuitoa kwa sababu ndugu zake wamekataa, ila kuiona nimeiona na siwezi kukwambia kwamba inasemaje"alisema mmoja wa watu wa karibu wanaoshugulikia taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja nchini Tanzania katika mahojiano maalumu na Habarimpya.com.
Habarimpya.com pia ilijaribu kuwasiliana na ndugu na jamaa wa Ngwea nchini Tanzania na kudai kwamba, ni kweli ripoti ya uchunguzo wa Madaktai umetoka lakini wao kama familia hawajaiona. "Nikweli tumesikia hivyo, lakini hatujui chochote kilichoandikwa na Madaktari, hivyo hatuwezi kuizungumzia, ingawa mimi pia siyo msemaji wa familia, lakini hata ukiwaona wahusika bado hawatakuwa na majibu yoyote kwa sababu wao wako Tanzania na ripoti bado iko Afrika Kusini"alisema mmoja wa wanafamilia wa marehemu ambaye hakutaja jina lake liandikwe ndani ya mtandao wa Habarimpya.com.

BEGI LA NGUO LAMTOA UHAI KIBAKA JIJINI DAR ES SALAAM LEO


Jamaa huyu asie na roho ya huruma akimmalizia mtuhumiwa na bonge la tofali! Tukio hili limetokea maeneo ya Mbagala Charambe mida ya saa sita mchana baada ya kibaka huyu kubahatika kukuta raia mwema kasahau kufunga mlango, Kibaka akazama ndani na kuchukua begi languo taratiiibu kama lake! Hakuridhika na begi alivyotazama pembeni akaona simu akaihifadhi mfukoni kiaina! Ile kutokanje tu akakutana na wenye nyumba uso kwa uso!!! Hapo ndipo mbio za marathon zilipoanza!!!!! Watu mwiziii mwiziiii mwiziiiiii mwiziiiiiiiiii!!!!! Jamaa akabahtika kujisweka kwenye jumba bovu lililoko uchochoroni na kuinusuru roho yake, Raia wenye hasira kali hawakumuona wakapita, Kufika mbele kidogo wakajadiliana na kukata tamaa wakati wakirudi majumbani kwao mara ghafla! Kurupu! Jamaa akachomoza kwenye dirisha la lile jengo bovu alilojificha, Harakati zikaanza upyaaaaaa!!!!! Aaaa... Anko jambazi hakuchukua raundi akatiwa mikononi...
Moto unawaka!
 Tairi limeletwa
 Anko jambazi ameveshwa tairi na kutiwa moto! Izraeli anapiga push up pembeni!!!


Shuhuli imeishia hapo

[ TOFAUTI KATI YA NDOA NA HARUSI ].



Katika pitapita zangu za udodosaji na upekuzi nimeona hili ni la maana sana kulipost katika page yetu tafadhali isome na uilewe ni funzo zuri sana kwa wote!

Tofauti ya NDOA na HARUSI:

Ndoa hazidumu kwa sababu kabla ya kufunga ndoa watu wanakuwa Obssesed na Wedding Ceremony Imaginations, bila kujua Ndoa inaenda mbali zaidi!

Kuna Ndoa na kuna Harusi...Wengi mnapenda zaidi harusi, na mnapowaza ndoa picha inayowajia ni Suti kali, Boonge la Shela kutoka Uturuki, Make Up ya ukweli ya bibi harusi kutoka Maznat Mikocheni, Mashosti kuingia ukumbini na Wimbo wa Alingo,Wanafiki kukomeshwa kwa jinsi pati yako itakavyokua kali pale Karimjee Hall..

Je, umewahi kuwaza Mmeo au mkeo akiumwa miaka 5 mfululizo utaweza kumvumilia?? Umewahi kuwaza Watoto watakapozaliwa na ulemavu utawa-care namna gani?? Mtakapokosa watoto miaka 6 ya ndoa utahimili maneno ya Mama Mkwe na Mawifi kwamba unawajazia Choo cha kaka yao na huna kizazi?? Ndoa ni zaidi ya Sherehe ya Harusi.

Baada ya yale Matarumbeta kuzimika usiku kifuatacho ni Majukumu mazito na Kiapo kisichovunjika. Achana na Fantasy za Kwaito,waza mbali kidoogo... Je, Uko tayari kuwa Mme au Mke wa mtu mmoja tu au Ma-Ex watarejea kidogo kidogo kama hupati Satisfaction ya kutosha kwa mumeo??? Huwa mnawaza hayo au mnawaza Zawadi ya Kamati itatoa Verossa ya kuanzia maisha?? Sidhani... Kabla ya kuoa na kuolewa jiulize,Unatamani Ndoa au ni tamaa ya Sherehe ya Harusi????

please like comment na share..

Credit- Mike Tee Senior

WABUNGE QUEENS WAFANYA KWELI KATIKA UWANJA WA JAMUHURI



mchezaji wa wabunge queens Halima Mdee akifurahia ushindi baada ya kuwafunga NSSF media