Marehemu Mangwea (kulia) enzi za uhai wake akiwa na msanii M 2 The
P,ambea pia alizimia akiwa na marehemu na kupata nafuu
Pretoria,Afrika Kusini
WATANZANIA wanaoishi nchini Afrika Kusini na nchi jirani ya
Botswana leo wamejitokeza kuuaga mwili wa Marehemu Albert Mangwea,kesho mwili
wa marehemu unatarajia kuwasili nchini Tanzania na kupelekwa katika Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili kuhifadhiwa, kabla ya shuguli za kuuaga tena kufanyika
katika Viwanja wa Leaders Club jijini Dar es Salaam.
Mangwea aliagwa na umati wa watu mbalimbali wakiwemo
Watanzania na watu wa mataifa mbalimbali wanaoishi nchini Afrika Kusini, jijini
Dar es Salaam pia kutakuwa na zoezi kama hilo siku ya Jumatatu kabla ya
kusafirishwa hadi mjini Morogoro kwa mazishi siku ya Jumanne.
Pamoja na kwamba Mangwea anatarajia kuzikwa mjini Morogoro,
utata juu ya ripoti ya uchunguzi wa kifo chake imeanza kutawala, baada ya
kuwepo kwa mvutano wa kuifanya ripoti hiyo kuwa siri, huku baadhi ya watu
wakitaka ripoti itangazwe kama ilivyoandikwa na jopo la Madaktari
wa Hospitali ya St Hellena Joseph.
Inaelezwa kwamba familia ya msanii huyo imekataa kuweka wazi
sababu za kifo cha mtoto wao, "Ripoti ya Uchunguzi wa Madaktari imetoka
lakini haturuhusiwi kuitoa kwa sababu ndugu zake wamekataa, ila kuiona nimeiona
na siwezi kukwambia kwamba inasemaje"alisema mmoja wa watu wa karibu
wanaoshugulikia taratibu za kusafirisha mwili wa marehemu kuja nchini Tanzania
katika mahojiano maalumu na Habarimpya.com.
Habarimpya.com
pia ilijaribu kuwasiliana na ndugu na jamaa wa Ngwea nchini Tanzania na kudai
kwamba, ni kweli ripoti ya uchunguzo wa Madaktai umetoka lakini wao kama
familia hawajaiona. "Nikweli tumesikia hivyo, lakini hatujui chochote
kilichoandikwa na Madaktari, hivyo hatuwezi kuizungumzia, ingawa mimi pia siyo
msemaji wa familia, lakini hata ukiwaona wahusika bado hawatakuwa na majibu
yoyote kwa sababu wao wako Tanzania na ripoti bado iko Afrika
Kusini"alisema mmoja wa wanafamilia wa marehemu ambaye hakutaja jina lake
liandikwe ndani ya mtandao wa Habarimpya.com.
No comments:
Post a Comment