![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiUFk7-9VJnmqFubZ8SFuh7BgmixBsamEFpgq0hazWfJg5ZE6a8LT0xYS1JVL1VXcWF_XCam1CDWJoe7vrOoOOB4IcIizvRqtSQfqiBybTSh-ZNpGIwLbUrNwEQZEaQpgCaBbgt1e1OOoo/s400/vimin.jpg)
RAIS Yoweri Museveni amesaini sheria ambayo inaharamisha mavazi yasiyo ya heshima na picha za utupu.
Pia, wanawake wamepigwa marufuku kuvaa nguo fupi - vimini na blauzi fupi – vitopu, ambavyo vinashawishi hisia za ngono, isipokuwa kama vivazi hivyo vitatumika kwa madhumuni ya kutoa elimu au matibabu au kutumika kwenye michezo na utamaduni.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika Kituo cha Habari jijini Kampala juzi,
Waziri wa Nchi anayeshughulikia Maadili, Mchungaji Simon Lokodo, alisema
Rais alisaini Muswada huo kuwa sheria Februari 6, miezi miwili baada ya
kupitishwa na Bunge Desemba mwaka jana.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu. Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miaka 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu. Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miaka 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.
Kwa
mujibu wa sheria hiyo, sasa itaundwa Kamati ya Taifa ya Kukabiliana na
Ukiukwaji wa Maadili ya Nchi, ambayo itakuwa na wajibu wa kubaini,
kukusanya na kuharibu vitu vyote vinavyohusiana na pon*grafia (picha au
maandishi yenye kutia ashiki).
Kamati
hiyo, ambayo wajumbe wake watatoka sekta mbalimbali zikiwamo tasnia za
habari na burudani, pia itatoa huduma za kurekebisha tabia kwa
waathirika wa ponografia.
Sheria
hiyo dhidi ya ponografia, inatengua na kuchukua nafasi ya Kifungu cha
166 cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, na kupanua wigo wa
tafsiri ya sheria ya pon*grafia na kuiharamisha.
Kwa
mujibu wa sheria hiyo, pon*grafia inamaanisha “chochote kitakachotolewa
kupitia chapisho, maonesho, filamu, teknolojia ya mawasiliano au kwa
njia nyingine yoyote, kinachoonesha mtu akiwa katika tendo halisia au
maigizo ya ngono au kuonesha sehemu za siri za mtu kwa ajili ya
kusababisha ashiki.”
Waziri
Lokodo pia alitaja matangazo mafupi ya ngono maarufu kama bimansulo,
video au picha za ngono kwa watoto, na wanamuziki, hususan wasanii wa
kike, ambao hucheza wakiwa wamevalia nguo fupi, kwamba navyo vimepigwa
marufuku.
“Hatupendi
mwonekane katika hali ambayo inavuta hisia za watu wengine. Kuweni na
staha na nguo zenu zikuonesheni kuwa watu wenye staha,” alisema Lokodo.
Alipotakiwa
kufafanua kuhusu uvaaji usio na staha, Waziri alisema: “Kama utavaa
vazi ambalo linatatiza fikra na kushitua watu wengine hususan wa jinsia
tofauti, umevaa vibaya na tafadhali harakisha kubadilisha vazi lako.”
Vituo
vya habari navyo vimepigwa marufuku, kuchapisha picha za watu wawili
wakibusiana au wanawake waliovaa vibaya kama wanaoonekana katika klabu
za usiku, kwa mujibu wa Patricia Achan-Okiria, Ofisa Mkuu wa Sheria
katika Wizara ya Maadili.
Waziri
huyo alielezea wasiwasi unaooneshwa na wabia wa maendeleo juu ya
muswada wa kupinga pon*grafia, kama jambo ambalo halitaweza kuiondoa
ofisi yake kwenye mapambano dhidi ya mmomonyoko wa maadili katika jamii.
No comments:
Post a Comment