Brighton Dama Zanthe, mwenye miaka 34, aliingizwa ndani ya jeneza Jumatatu baada ya kuwa amefariki nyumbani kwake baada ya kuugua kwa muda mrefu. Lakini siku iliyofuata marafiki wa Zanthe na jamaa zake walisambaratika wakiwa hawaamini pale alipoanza kutembea wakati wakipita mbele ya jeneza kuaga mwili wa ‘marehemu’ huyo. Bosi wa ‘marehemu’ huyo, Lot Gaka alieleza kuhusu mkasa huo alipobaini mfanyakazi wake alikuwa bado angali hai.
Alisema: “Kwanza niligundua miguu ya Zanthe ikisogea wakati nilipokuwa kwenye ya foleni kutazama mwili wake. Hili lilinishitua mno. Kwanza sikuweza kuamini macho yangu lakini baadaye nilibaini kwamba kulikuwa na kusogea kwa viungo kadhaa katika mwili wake huku waombolezaji wengine wakiwa hawaamini kinachoendelea.”
No comments:
Post a Comment