Mtayarishaji
wa Muziki wa Bongo Fleva Prof Ludigo alieshirikiana na P Funk Majani
kutengeneza Wimbo wa Mikasi wa Marehemu Albert Mangwear ametoa lawama
kwa Radio ya watu Clouds Fm kuwa uongozi wake ndio umekuwa chanzo
kikuu kusababisha kifo cha Msanii Mangwea aliefariki kwa kutumia
madawa ya Kulevya.
Prof
Ludigo katika ujumbe wake aliomtumia P funk akimtaka ampe Taarifa
Mmiliki wa Radio Hiyo Kusaga Kuwa hataki kusikia wimbo wa Mikasi
Ukichezwa katika Radio hiyo kwa kudai kuwa wao ndio wamemtumia vibaya
msanii huyo na kumfanya aingie kwenye matumizi ya madawa ya kulevya
kama njia moja wapo wa kupunguza mawazo aliokuwa nayo mpaka umauti
umemkuta jana.
Ludigo
amesema kuwa hakufanya jambo lolote enzi za Uhai wa msanii huyo kwa
sababu alihofia gharama za kuishi mjini kwa msanii huyo aliekuwa
akitumiwa na watu hao katika kazi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment