HUKU akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na
madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald
‘Masogange’ amepata balaa jipya,GUMZO LA JIJI lina taarifa kamili...
Dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo, Masogange
na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo
wamerudi tena rumande.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
KWA NINI DHAMANA IFUTWE?
Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili
hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini
huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama
jaribio la kuikimbia kesi hiyo.
“Unajua huku Sauzi si kila mtu
anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa
utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila
kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni
‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.
“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange,
wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua
jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo
ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu
wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.
“Hii
inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na
kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa,
ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea
maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.
MASOGANGE AKAUKA MITANDAONI
Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea
kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini
baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
“Nyiye si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale
katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa
yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.
WABONGO WALIOJITOLEA FEDHA KUMWOKOA WASIKITIKA
Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya
Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha
kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za
kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.
Kamanda Nzowa.
SHERIA ZA AFRIKA KUSINI NA TANZANIA KUHUSU ‘UNGA’ SI SAWA?
Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza
kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani,
Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande.
POLISI HAWAKAUKI NYUMBANI KWAKE
Habari kutoka vyanzo vya hapa Bongo zinadai kuwa, askari polisi (kituo
cha kazi hakijajulikana) wamekuwa wakifika nyumbani kwa msanii huyo,
Kijitonyama, Dar na kuwauliza mambo kadhaa majirani.
“Jamani ishu ya
Masogange vipi? Maana hapa mtaani kuna polisi wamekuwa wakija mara kwa
mara na kumuulizia kama yupo. Wao hawajitambulishi kama askari lakini
watatu kati yao wamebainika ni polisi,” kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea kudai kuwa, Julai 20, mwaka huu alifika askari mmoja na
kuuliza majirani kama wamewahi kumwona mwanaume mrefu, mweupe akiingia
kwenye nyumba ya Masogange.
“Julai 20 alikuja afande mmoja,
akawauliza majirani kama kuna siku yoyote ambayo mwanaume mrefu, mweupe
aliingia kwa Masogange, akajibiwa hajawahi kufika mtu wa aina hiyo.
“Ndiyo maana nikauliza kesi yake vipi kule Bondeni (Afrika Kusini)? Ila
kuna kitu nilikisikia kwa baadhi ya watu kwamba kuna ndugu yake atakuja
kuhamisha vyombo vyake kwa sababu wanajua kesi itachukua muda mrefu,”
kilisema chanzo.

Masogange.
KUMBUKUMBU
Julai 5, mwaka huu, Masogange na Melisa walinaswa na
madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo
mjini Kempton Park, Afrika Kusini.
Ilidaiwa kuwa thamani ya mzigo huo wenye kilo mia moja na hamsini ni shilingi bilioni moja na laki sita..