Saturday 21 September 2013

HAPPINESS WATIMANYWA AIBUKA KIDEDEA REDD'S MISS TANZANIA 2013.


Redd's Miss Tanzania 2013,Happiness Watimanywa akipungia mkono mara baada ya kutangazwa mshindi wa Taji hilo kwa mwaka huu.Kushoto ni mshindi wa pili,Latifa Mohamed na kushoto ni mshindi wa tatu,Clara Bayo.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakiwa jukwaani usiku huu wakati wa Onyesho la Taifa la Urembo linalofanyika kwenye Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakifungua shindano la mwaka huu kwa kuonyesha ufundi wao wa kucheza muziki. Shindano la mwaka huu ambalo limedhaminiwa na kampuni ya vinywaji Tanzania.Tanzania Breweries Limited kupitia kinywaji cha Redds limefanyikia katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar-es-salaam. Jumla ya warembo 30 kutoka mikoa mbalimbali,vyuo nk wameshiriki.

 Warembo walioingia hatua ya kumi na tano bora. 
 Jaji Mkuu wa Shindano la Redd's Miss Tanzania,Dkt. Ramesh Shah akitangaza Warembo walioingia hatua ya tano bora.
Warembo walioingia hatua ya tano bora,toka shoto ni Happiness Watimanya,Elizabert Peter,Clara Bayo,Lucy Tomeka pamoja na Latifa Mohamed.
 Warembo wa Redd's Miss Tanzania 2013 wakipita jukwaani na mavazi ya aina mbali mbali wakati wa Onyesho la Taifa Redd's Miss Tanzania 2013 linalofanyika usiku huu kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam usiku huu. 
Mwanamuziki Mkongwe wa Muziki wa Kizazi kipya hapa nchini,Lady Jay Dee akitoa burudani kwenye Onyesho la Redd's Miss Tanzania 2013,linalofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mlimani City,jijini Dar es Salaam. 

Thursday 19 September 2013

RIPOTI YA KUHUSU KUACHIWA HURU KWA AGNES MASOGANGE NA MELISA HUKO AFRIKA KUSINI




WATANZANIA wawili, Agnes Gerald (Masogange) na mwenzake Melissa Edward waliokamatwa nchini Afrika Kusini kwa madai ya kusafirisha kilo 150 za dawa za kulevya wanayo nafasi kubwa ya kuachiwa wakati wowote kuanzia sasa, Raia Mwema limeambiwa.
  
Ingawa ripoti za awali zilieleza kwamba Watanzania hao walikuwa wamesafirisha kilo 150 za dawa aina ya Crystal Methamphetamine zenye thamani hiyo nchini Afrika Kusini wakati zikisafirishwa kutoka Tanzania, imebainika kwamba adawa walizobeba zinafahamika kwa jina la Ephedrine ambazo hazimo katika kundi la dawa za kulevya.
  
Watanzania hao walikamatwa nchini Afrika Kusini katika Uwanja wa Ndege wa Oliver Tambo jijini Johannesburg wakiwa na dawa hizo zilizokadiriwa kuwa na thamani ya Sh bilioni 6.8.
  
Hata hivyo, Ephedrine –dawa ambayo sasa imebainika kuwa ndiyo waliyosafirisha akina dada hao inaangukia katika kundi la vibashirifu (precursors) yaani dawa ambazo malighafi yake inaweza kutumika kutengeneza dawa za kulevya.
  
“Kusema kweli nguvu ya kesi ya akina Masogange imepungua sana mara baada ya kubainika aina ya dawa walizokuwa nazo. 

"Kama zingekuwa ni dawa za kulevya, mambo yangekuwa mengine lakini kwa haya waliyokamatwa nayo, sidhani kama kuna kesi ngumu sana. Nataraji watapewa dhamana wakati wowote kutoka sasa,” kilisema chanzo cha kuaminika cha gazeti hili ndani ya Jeshi la Polisi. 

Masogange na mwenzake wanashikiliwa nchini Afrika Kusini tangu Julai, mwaka huu.

Kwa mujibu wa Sheria ya Dawa za Kulevya ibara ya 26 (1) a na b, dawa zinazotambulika kama za kulevya hapa nchini ni kama vile Cocaine, Heroin, Mandrax, Bangi, mirungi na nyingine lakini ephedrine haimo katika kundi la dawa za kulevya.
  
Ni sheria hiyo ambayo imetamka wazi kwamba mtu anayekamatwa na dawa hizo zikiwa na thamani ya zaidi ya Sh milioni 10 haruhusiwi kupewa dhamana lakini zikipungua thamani hiyo, anaweza kupewa dhamana.
  
Vyanzo vya Raia Mwema vimebainisha kwamba kwa vile Ephedrine si dawa za kulevya kwa mujibu wa sheria zilizopo, watuhumiwa hao wanaweza kupewa dhamana.
  
Kwa mujibu wa mwongozo wa wadau wa mapambano dhidi ya Dawa ya Kulevya uliotolewa mwaka 2011, uingizwaji na matumizi ya dawa kama hizo zinazofahamika kwa jina la vibashirifu, unatawaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
  
Gazeti hili lilipiga hodi katika ofisi za TFDA jijini Dar es Salaam ambako lilielezwa kwamba vibashirifu huingizwa nchini kwa utaratibu maalumu kulingana na mahitaji ya kitaifa yaliyopo.
  
“Unapozungumzia vibashirifu, unazungumzia mambo ya kitaalamu. Nitakupa mfano, kuna mmea unaitwa Coca. Mmea huu unatengeneza dawa za kulevya zinazofahamika kwa jina la cocaine lakini ni mmea huo huo ndiyo unatengeneza soda ya Cocacola ambayo karibu kila mtu anatumia.

“Mtu anaweza kutumia Ephedrine kutibu magonjwa kama vile mafua lakini anaweza kuitumia pia kama dawa za kulevya. Unajua baadhi ya dawa zilizo kwenye kundi la dawa za kulevya zinatumika pia hadi kwenye hospitali mbalimbali lakini kwa shughuli na kiwango maalumu.
  
“Mtu akitaka kuagiza dawa hizo ni lazima apate kibali kutoka kwetu. Tukizikamata kwa mtu ambaye hana kibali tunaziteketeza. 

Hiyo ndiyo adhabu ya kwanza lakini kama kutaonekana kulikuwapo na nia ya uhalifu, basi mkono wa sheria utachukua mkondo wake, alisema mmoja wa maofisa waandamizi wa TFDA aliyezungumza na gazeti hili kwa masharti ya kutotajwa jina kwa kuwa si msemaji rasmi wa mamlaka hiyo.

Kwa mujibu wa mtandao wa Wikipedia, matumizi ya Ephedrine yalianza nchini China miaka zaidi ya 200 Kabla ya Kristo na inapatikana sana katika mmea wa Ma Huang ambao unatumika kutibu magonjwa mbalimbali katika tiba za Kichina.
  
Mwaka 1994, aliyekuwa nahodha wa timu ya soka ya taifa ya Argentina, Diego Maradona, aliondolewa kwenye mashindano ya Kombe la Dunia nchini Marekani na baadaye kufungiwa kucheza soka baada ya kukutwa na hatia ya kutumia Ephedrine ambayo ni miongoni mwa dawa zilizopigwa marufuku michezoni.
  
Raia Mwema limekosa taarifa za kwa nini vyombo vyote vya habari vya Afrika Kusini viliripoti kwamba dawa walizokutwa nazo zilikuwa ni Methamphetamine lakini sasa taarifa mpya zinataja kuwa ni Ephedrine.

Hata hivyo, nyaraka tofauti ambazo gazeti hili limezipata zinaonyesha kwamba Ephedrine na Methamphetamine zinafanana kila kitu tangu kwenye muundo wa molekyuli (chembe) zake isipokuwa Ephedrine ina kitu kinachoitwa Hydroxil ambacho hakipo kwenye Methamphetamine.

Akizungumza na gazeti hili kuhusu taarifa hizi mpya, Mkuu wa Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa, alisema anafahamu kuhusu hilo lakini wao wanaendelea na upelelezi wao kuhusu watu waliowatuma akina dada hao kupeleka dawa hizo nchini Afrika Kusini.
  
“Haya mambo yanafanyika huko Afrika Kusini na sisi hatuwezi kuingilia labda kama wakitaka kitu kutoka kwetu. Cha msingi kwetu ni kwamba dawa hizo zilitoka kwetu na wasichana wale hawana uwezo wa kuwa na mzigo wenye thamani ile. 

Tunawatafuta wahusika na tukipata taarifa tutawapa,” alisema Nzowa ambaye anatajwa kujijengea heshima kubwa kwenye vita hii dhidi ya dawa ya kulevya. 

Source:Raia Mwema

Tuesday 3 September 2013

CHADEMA WAMKANA AFANDE SELE....WADAI HAWAJAWAHI MUOMBA AGOMBEE UBUNGE MOROGORO


Gazeti la Habari Leo la siku ya leo tarehe 2 Septemba lenye kichwa cha habari "Chadema kuzoa wasanii mastaa" pamoja na mambo mengine, mwandishi amemnukuu mmoja wa wasanii toka mkoa wa Morogoro akisema amewahi kuombwa na viongozi wa mkoa wa CHADEMA kugombea Ubunge. 

NAOMBA KUWEKA KUMBUKUMBU SAHIHI.
1. Mimi ndiye mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Morogoro, ninayeongoza Baraza la Uongoz la mkoa lenye wajumbe wa5 tu tangu mwaka 2009. 
2. Katika vikao vyetu vyote hukujawahi kuwepo kwa AGENDA ya kumuomba/ kumshawishi mtu yeyote kugombea nafasi yoyote. 
3. Hatujawahi kumuomba Afande Sele kugombea. Mbali na hilo hatujawahi hata kumuomba tu kujiunga na CHADEMA.  
  4. Kwa upande wa gazeti la Habari leo, naungana na kauli ya JB kwamba, kuna dalili za wazi kwamba habari hii imepikwa na mwandishi mwenyewe. 

Asanteni Makamanda.
PUUZENI TAARIFA HII Susan Limbweni Kiwanga

DIAMOND NA LINAH SANGA NDANI YA MAPOZI YA UTATA KWA MARA NYINGINE TENA


Tabia mbaya! Staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amenaswa na msanii mwenzake, Esterlina Sanga ‘Linah’ wakiwa kwenye mapozi ya kimahaba ambayo yametafsiriwa vibaya

Katika tukio hilo lililojiri juzikati kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora ndani ya Tamasha la Serengeti Fiesta, Diamond alishuhudiwa akiwa amempakata Linah ndani ya basi huku mikono ya jamaa huyo ikishika maeneo nyeti.
Mara baada ya kutimba uwanjani hapo wakitokea hotelini tayari kwa kufanya shoo, Diamond na Linah walibaki kwenye basi wakiwa wamepakatana na hata msichana huyo alipomaliza shoo yake kali mishale ya saa 3: 00 usiku, alirejea mikononi mwa Diamond ambaye alimpachika mapajani

Shushushu wetu aliwapiga chabo ‘wakifanya yao’ hadi Diamond alipokwenda stejini na kuangusha bonge la shoo huku akimwacha Linah mpweke.
Kwa mujibu wa mashuhuda, kama kweli mchumba wa Diamond, Penniel Mungwilwa ‘Penny’ anakubali mambo kama hayo, basi atakuwa na roho ngumu au moyo wa chuma.



Mwanahabari wetu alipomuuliza Linah kuhusu ishu hiyo, alifunguka: “Weweee…hakuna ni mapozi tu na wala usiandike hiyo habari.”
Siyo mara ya kwanza Diamond na Linah kuripotiwa wakiwa wamepozi kimahaba kwani mwaka jana walifanya hivyo wakiwa jijini Mbeya hivyo kutafsiriwa kuwa inaonekana ni katabia kao kabaya wanakaendekeza.

SOURCE: GPL

CHUPI NA SHANGA ZA MSANII SHILOLE ZAANIKWA NJE- FIESTA

Dance imekolea kwa shilole hapo ...mpaka mambo yote hadharani ......kitu cha black

HIVI WEMA ALIMKOSEA NINI DIAMOND, KAMPIGA TENA KIJEMBE KWENYE WIMBO WAKE MPYA

Leo video ya muziki ya Msanii Diamond platnumz ya wimbo wa My Number one imetoka rasmi kwenye Television na mitandao mbalimbali ya kijamii na kusema ukweli ni moja ya video nzuri sana za muziki hapa nchini na sio siri kijana huyu wa bongofleva amefanya kazi kubwa sana na anastahili pongezi.

Baada ya kuisikiliza kwa makini nyimbo hii yenye mahadhi flani ya kiafrika zaidi tulifika kwenye dakika ya 2 na sekunde 50 (2:50) ya nyimbo hii na ndipo ukatokea “ubishi” ambao tukaona sio mbaya tukiupeleka kwa wasomaji wetu ili kupata maoni Zaidi.

Katika sehemu hii ya mwisho ya nyimbo hii Diamond anatamka maneno ambayo baadhi ya watu tuliokuwepo katika mabishano hayo tunasema kuwa yanamlenga mwanadada wetu muigizaji, Wema sepetu kama “vijembe” kwakwe, diamond anamalizia wimbo wake kwa kusema “TUACHE TULALE” maneno amabyo kwa wale wanafuatilia habari za watu hawa wawili yalioongewa na mpenzi wa diamond wa sasa VJ penny kwenye tukio la wapenzi hao kumrekodi mwanadada Wema Sepetu kwenye simu alipokuwa akimbembeleza mpenzi wake wa zamani (Diamond Platnumz) warudiane, tukio liliotokea miezi kadhaa iliyopita.

Swali likawa, Je maneno haya yatakuwa yanamlenga Wema??? Kama siyo kwanini Diamond ayatamke sehemu ambayo hata haihusiani nayo kwenye wimbo???