Monday 29 July 2013

AZZAN:NITAJIUZULU IKIBAINIKA NIUZA MADAWA YA KULEVYA



MBUNGE wa Kinondoni (CCM), Idd Azzan, amesema yupo tayari kujiuzulu ubunge, ikiwa itabainika anajihusisha biashara ya dawa za kulevya. Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya kutajwa katika moja ya barua iliyosambazwa katika mitandao ya kijamii, baada ya mtu anayedaiwa kukamatwa China na kuwatuhumu watu kadhaa akiwamo Idd Azzan. Akizungumza na MTANZANIA jana kuhusu sakata hilo, alisema hatua ya kuhusishwa na biashara haramu ya dawa za kulevya, ni kutotenda haki mbele ya jamii hasa wapiga kura wake na Taifa kwa ujumla.

Alisema mtu aliyendika barua ya tuhuma dhidi yake, ni wazi amedhamiria kumshushia heshima na huenda akawa ana jambo limejificha.

“Ni kweli nimeiona hiyo barua katika mtandao, inayodaiwa imeandikwa na kijana ambaye amekamatwa Hong Kong nchini China. Lakini ninajiuliza kama kweli yeye ni raia mwema, katika hili kwanini hakutaka kutaja jina lake kwenye barua hiyo.

“Hata nilipoisoma nimebaini kuwa huyo mtu ametumika na huenda kabisa hayupo nje ya nchi, kwani katika maelezo yake anataja jina la Balozi Philip Marmo kuwa amemsaidia hali ya kuwa hivi karibuni Rais Kikwete alimteua Balozi mpya Abdulrahman Shimbo na Marmo kuwa Balozi wa Shirikisho la Ujerumani.

“Kingine naona alijaribu kuandika uongo kuweza kuaminisha jamii, kwani hata hilo jila la balozi mwanzo limetajwa jina la Bernad na kukatwa kwa wino. Ninapenda kulieleza Taifa kuwa naomba vyombo vya usalama vifanye uchunguzi wa jambo hili na nikibainika ninauza dawa za kulevya nipo tayari kujiuzulu ubunge wangu.

“Kubwa haki itendeke katika kufanya uchunguzi wa jambo hili, ila ni lazima jamii na Watanzania kwa ujumla tusikubali kwa makusudi watu waichafue nchi yetu kwa chuki na fitna tu,” alisema Azzan.

Alisema kutokana na hali hiyo, anashindwa kuchukua hatua yoyote ya kufanya zaidi ya kuliandikia barua Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi dhidi ya barua hiyo kuweza kubaini ukweli wa jambo hilo.

“Sijawahi kuuza dawa za kulevya na hata katika familia yangu hakuna mtu anayefanya biashara hiyo haramu. Kila mmoja anajua kuwa Idd nilikuwa Diwani wa Kata ya Magomeni, huku kazi yangu kubwa ikiwa ni biashara ya magari na daladala ambayo ninaendelea nayo hadi sasa mbali ya ubunge kama nilivyopewa heshima na wapiga kura wangu wa Kinondoni,” alisema Azzan.

MTANZANIA ilipomuuliza kuwa ni hatua gani ikibainika hakuna ukweli wa jambo hilo baada ya vyombo vya usalama kufanya uchunguzi, alisema atakachokifanya anamuachia Mungu.

“Ni ngumu kusema hatua gani nitachukua ikibainika hakuna ukweli, lakini nataka kusema kama yule aliyeandika barua hii angetaja jina lake ni wazi baada ya uchunguzi ningeweza kuomba ushauri kwa mwanasheria wangu hatua za kuchukua, lakini kwa kuwa hakutaja jina ni ngumu kuweza kuamua,” alisema Azzan.

Kwa mujibu wa taarifa zilitolewa kupitia mitandao, ziliripoti kukamatwa kwa Watanzania wawili nchini China wakiwa na dawa za kulevya zenye thamani ya Dola milioni 3.34 za Marekani.

MASOGANGE BALAA JIPYA,MAHAKAMA YAMFUTIA DHAMANA ARUDISHWA LUPANGO


HUKU  akiwa hajui nini hatima ya kesi inayomkabili ya kunaswa na madawa ya kulevya nchini Afrika Kusini, Video Queen Agnes Gerald ‘Masogange’ amepata balaa jipya,GUMZO LA JIJI lina taarifa kamili... 
   

 

                          Dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa chanzo chetu makini ambacho kipo nchini humo, Masogange na mwenzake aliyekamatwa naye, Melisa Edward wamefutiwa dhamana hivyo wamerudi tena rumande.
Agnes Gerald ‘Masogange’.
KWA NINI DHAMANA IFUTWE?
Habari zinadai kuwa, dhamana za wawili hao zimefutwa kufuatia kuhisiwa kwamba wana mpango wa kuondoka nchini huko kinyemela na kurejea Tanzania, jambo ambalo limetafsiriwa kama jaribio la kuikimbia kesi hiyo.
“Unajua huku Sauzi si kila mtu anawaonea huruma Masogange na Melisa kwa tatizo lililowapata, sasa utakuta maskani mtu anaropoka vitu vya ajabu pengine vya uongo bila kujua kuwa si kila mtu anayesikiliza atayaachia hapohapo, wengine ni ‘mainfoma’ wanayafikisha mbele.

“Hicho ndicho kilichomtokea Masogange, wakati baadhi ya watu wakiwa kwenye mchakato wa kumsaidia ili kujua jinsi gani kesi yake itakwenda haraka, wengine wanakwenda kuongea mambo ya ajabu kwa watu wao wanaowatuma kuwapelekea taarifa, eti kuna watu wanajipanga kuwatorosha, si sheria ikafuata mkondo wake.
“Hii inatupa wakati mgumu sisi tuliokuwa tumsaidie, mara kwa mara tunaitwa na kuhojiwa na jeshi la polisi. Ndiyo maana dhamana yao imefungwa, ukiangalia nini kilichosababisha ni maneno ya uongo yanayotokea maskani,” kilisema chanzo hicho ambacho kiliomba hifadhi ya jina lake.

MASOGANGE AKAUKA MITANDAONI
Licha ya kukumbana na kesi ya madawa ya kulevya, Masogange aliendelea kutumbukiza picha zake kwenye mitandao ya kijamii na kuzielezea, lakini baada ya kufutiwa dhamana amekauka mitandaoni kwa picha za karibuni.
“Nyiye si mnaona, siku hizi haposti tena picha zake mpya kama palepale katikati baada ya kukamatwa. Siku zile alikuwa nje kwa dhamana, sasa yupo rumande hawawezi kumwachia akacheza na simu,” kilisema chanzo.

WABONGO WALIOJITOLEA FEDHA KUMWOKOA WASIKITIKA
Baada ya staa huyo kutiwa nguvuni Julai 5, mwaka huu, baadhi ya Watanzania waishio Bongo na kule Afrika Kusini walidaiwa kuchanga fedha kwa lengo la kumsaidia mrembo huyo lakini kufuatia kuvuja kwa taarifa za kufungwa kwa dhamana yake, wamekosa nguvu na kusikitikia kitendo hicho.
Kamanda Nzowa.
SHERIA ZA AFRIKA KUSINI NA TANZANIA KUHUSU ‘UNGA’ SI SAWA?
Inadaiwa kuwa, nchini Afrika Kusini mtu akikamatwa na ‘unga’ anaweza kuwa nje kwa dhamana wakati kesi yake ikiendelea kusikilizwa mahakamani, Tanzania mtu akinaswa na unga kesi inasikilizwa akiwa rumande.

POLISI HAWAKAUKI NYUMBANI KWAKE
Habari kutoka vyanzo vya hapa Bongo zinadai kuwa, askari polisi (kituo cha kazi hakijajulikana) wamekuwa wakifika nyumbani kwa msanii huyo, Kijitonyama, Dar na kuwauliza mambo kadhaa majirani.
“Jamani ishu ya Masogange vipi? Maana hapa mtaani kuna polisi wamekuwa wakija mara kwa mara na kumuulizia kama yupo. Wao hawajitambulishi kama askari lakini watatu kati yao wamebainika ni polisi,” kilisema chanzo hicho.
Kiliendelea kudai kuwa, Julai 20, mwaka huu alifika askari mmoja na kuuliza majirani kama wamewahi kumwona mwanaume mrefu, mweupe akiingia kwenye nyumba ya Masogange.
“Julai 20 alikuja afande mmoja, akawauliza majirani kama kuna siku yoyote ambayo mwanaume mrefu, mweupe aliingia kwa Masogange, akajibiwa hajawahi kufika mtu wa aina hiyo.
“Ndiyo maana nikauliza kesi yake vipi kule Bondeni (Afrika Kusini)? Ila kuna kitu nilikisikia kwa baadhi ya watu kwamba kuna ndugu yake atakuja kuhamisha vyombo vyake kwa sababu wanajua kesi itachukua muda mrefu,” kilisema chanzo.
Masogange.
KUMBUKUMBU
Julai 5, mwaka huu, Masogange na Melisa walinaswa na madawa ya kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo mjini Kempton Park, Afrika Kusini.
Ilidaiwa kuwa thamani ya mzigo huo wenye kilo mia moja na hamsini ni shilingi bilioni moja na laki sita..

DIAMOND PLATNUMZ AENDA SHULE SOUTH AFRICA KUONGEZA VIDATO


The Bongo Flava Prince, Diamond Platnumz yupo nchini Afrika Kusini alikoenda kuongeza vidato kidogo. Apparently, hitmaker huyo wa Kesho amejiunga na chuo ambacho hakijajulikana jina lake bado na hajasema ameenda kusoma nini.

Kupitia Facebook, staa huyo amewauliza mashabiki wake wabashiri ameenda kusoma nini chuoni hapo na haya ni baadhi ya majibu.

Faiso Yahya: Ka si english course basi unenguaji

Galus de Focus: HOTEL MENEGEMENT

Benjamin Osarya Jr.: Unasoma matangazo….kwenye notes board.

Nelson Choka: Samahan form 4 umemaliza ww et..!! Labda una risit dogo mh

Rose Selestini: Unatafuta wadada wa chuoni.

Christian Biseko: wa kusoma uwe wewe??? Elimu siyo mchezo wewe!!!

Gara B Kubwa: English Course ili Ushiriki BBA mwakani…una Mbwembwe dogo wewee..

Emmanuel Makaga: Unasomea jnc ya kubun skendo mpya kwny mass media

Gabrie Lbrighton: Wanaosoma hawajitangazi wew may be ungetuambia akitoka huyu mwanamke uliye nae nani anafata.
Nàdhifá Dórnald Unasomea mapenz maana unayapenda sana

Sunday 28 July 2013

SOMA BARUA ILIYOANDIKWA NA MFUNGWA WA MADAWA YA KULEVYA KUTOKA TANZANIA HUKO HONG KONG-MBUNGE KATAJWA

Below is one drug mule story, the story of mules from Tanzania entering Hong Kong. Because of its location on the East coast of Africa, Tanzania is the favorite launching place for drug lords to mission their mules. The drugs they carry are mainly from Pakistan and Afghanistan....taken by boat to Tanzania ....meeting small boats along Tanzania's long coastline

In Hong Kong there are currently about 200 inmates from Tanzania. About 130 convicted and about 70 on remand  (...unofficial figures..). In May-June 2013, some 50 Tanzanians were arrested in Hong Kong and China

Those convicted serve a minimum time of about 9 years if they plead guilty. They serve 21 years if they don't plead guilty (but drugs are found in their possession)

The story of these Tanzanian mules entering Hong Kong is typical of what happens around the world. Hopefully this story will be seen by many people in Africa, especially in Tanzania, and will discourage others from becoming mules. If this article stops even one person from being a mule, it is worthwhile
 Here is the story, written in Swahili by a Hong Kong Tanzanian inmate, translated into English by another inmate. The story names and shames some very important people in Tanzania:





Wednesday 24 July 2013

JEURI YA FEDHA WEMA SEPETU AVUTA MKOKO UNAOENDANA NA RANGI AIPENDAYO ZAIDI KATIKA MAISHA YAKE


Haya ndio Maneno ya Martin Kadinda aliyoandika facebook na kuweka picha ya Wema akiwa na gari hilo

"samahani kwa ubora wa picha kuwa hafifu....... Ila huyu dada anapenda pink kupitiliza..... haya she gat new pink Car.... mkutane barabarani..." aliandika Martin

CHRISTINA ADEL ATISHA MAMODEL WOTE BONGO............

CHRISTINA ADEL (21) alietoa kauli kali kwa wrimbwende wote Tanzania kua hana mchezo wala masihara na kazi sasa amekuja na moto mkali.
mrembo huyo anaefanya vizuri kwenye kazi za modeling ndani na nje ya nchi amefanya kazi nyingi zikiwemo KALI ELEGANCE SHOW, DAR FASHION FESTIVALPHOTOSHOOT na NIDA TEXTILE SHOW.
Mrembo huyo aliongea hayo alipokua akihojiwa na mwandishi wetu Arnold Adel jr makao makuu ya ofisi zetu. alinukuliwa akisema " Sina masihara na kazi hivo wanafanya modeling wajipange tena sana, HAPANA CHEZEA CHRISTINA WEWE......






Saturday 20 July 2013

BAADA YA KUFUTURISHA,DIAMOND ASOMA DUA NYUMBANI KWAKE...

Huu ulikuwa wakati maalumu kwaajili ya Dua takatifu kumuomba
Mwenyezi Mungu Rehema zake zitawale juu yetu
na kutuepusha na mabaya ya dunia na kutufanyia wepesi kwenye
 maisha yetu ya kila siku sambamba na
kuwaombea wasiojiweza,yatima,wajane,wagonjwa na vilema...


Namshukuru
Mungu kwa kufanikisha jambo ili kwenda
kiufasaha zaidi,napenda pia kumshukuru kila mmoja alieweza
kujumuika na mimi na familia yangu
kufanikisha dhifa hii........

Napenda kuchukua nafasi hii kukujuza kwa picha mtu wangu
wa kweli waeza cheki picha za tukio zima wakati
wa Dua inasomwa nyumbani, home sweet home kwa mama Naseeb Sinza......







Kisomo kikiendelea.....


Bi Sandrah akitia ubani....
Dada yangu Queen Darlene akitia ubani....
Hamza Bala....
Ommy Dimpoz akukosa nae kama mtoto wa kiislamu....
Rama tonser....


Shetta akukosekana wakati wa kusoma dua hii.....
Twinsfashion....
Nikiweka ubani kuitimisha Dua hii kama mlengwa...
Emma & Emma Platnumz usishangae hawa wote ndo majina yao....



Dianna dada ake mimi & Mama yangu mimi Bi Sandrah....

Rommy Jones akiwashukuru wageni kwa kujumuika nasi
siku ya leo kwenye Futari na kisomo

Nikitoa sadaka kwa watoto wanaolelewa kwenye kituo cha watoto yatima waliofika kufturu
nami nyumbani kwangu kidogo nipatacho basi mungu amenijaalia niweze kugawana nao..











Kutoka nje nikakutana na Dad G,Guru G Love alikuwa
amefika muda lakini kutokana na Dua kuendelea
ndani atukupata muda wa kusalimiana....
Kutoka kushoto,Ommy Dimpoz,Shetta the Don,Producer Nguli
 nchini Tanzania mi namuita Dad G wewe
waeza muita Dad pia au Guru G Love na mimi mwenyewe waeza
nihita Naseeb au kichwa kama mama
yangu aniitavyo....
Mapenzi tele kwa watoto hawa waliojumuika nami hakika
mwenyezi mungu awabariki
na azidi kuwaongoza katika njia zake....


Baada ya Dua nikiteta jambo na Ustaadh akinipa
mawaidha mawili matatu juu ya mwezi huu mtukufu